Home Uncategorized Naomi Osaka amkalisha Serena Williams katika fainali iliyojaa mvutano Us Open

Naomi Osaka amkalisha Serena Williams katika fainali iliyojaa mvutano Us Open

8764
0

Kama ulikuwa haufahamu Naomi Osaka anavutiwa zaidi kwenye tennis na Serena Williams na mwaka 2014 alihangaika sana kukutana na Serena ili tu kupiga naye picha (selfie) kama kumbukumbu.

Lakini usiku wa kuamkia leo mwanadada huyo mwenye asili ya nchi mbili Japan na Haiti alifanikiwa kuibuka kidedea zidi ya shujaa wake kwa ushindi wa seti 6-2, 6-4.

Naomi Osaka sasa anakuwa Mjapan wa kwanza kuwahi kushinda michuano ya US Open na anashinda michuano hii huku akiwa na miaka 20 tu.

Haikuwa mechi rahisi hata kidogo kwa Williams kwani mda mwingi alionekana kubishana na waamuzi hali ambayo ilimfanya kuonekana anapoteza focus kila wakati.

Mashabiki waliokuwa uwanjani walionekana wakimzomea Serena kila wakati kutokana na vitendo vyake katika mchezo huu na huku mwanadada huyo kudai US Open wamekuwa wakimfanyia hivi mara kwa mara.

Wadau wengi wa tennis wamekuwa na maoni kuhusu mchezo huu huku bingwa wa zamani wa Us Open Andy Roddick akisema huu ni mchezo uliokuwa na maamuzi mabovu zaidi kuwahi kuuona.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here