Home Kimataifa Nani wa kumzuia Man City?

Nani wa kumzuia Man City?

5785
0

Na Robert Komba

Kwa Mara nyingine tena wakicheza dhidi ya Bournemouth, Manchester city wanapata ushindi wa mabao 3-1. Ni ushindi wa 12 katika mechi 14 za EPL. ushindi ambao unazidi kuwaimarisha kileleni mwa ligi. Kitu cha kuvutia zaidi kwa upande wa city, sio takwimu zao tu Bali ni namna wanavyoweza kuwatala michezo katika hatua zote (kushambulia, kuzuia pamoja na vipindi vya mpito).

Katika mechi ya Leo city walionekana kuwa na umiliki mkubwa wa mpira toka mwanzo wa mchezo, kitu ambacho kilisababisha “the cherries” kurudi nyuma na kuzuia nafasi katika eneo la nyuma, muundo wao wakati wa kuzuia ulibadilika na kuwa 5-4-1 badala ya 3-4-3. Lakini kama ilivyo kawaida ya Kocha Eddie Howe aliwataka Cherries wasogee mbele kwa kuanza kujenga mashambulizi kutokea nyuma wakiwa na faida ya mabeki watatu wa kati walianza kufanya hivyo na taratibu defensive block yao ikasogea mbele kidogo ya eneo la hatari. Hii iliwafanya city waweze kutumia nafasi iliyoachwa nyuma ya mabeki wa mwisho (Mings, Ake na Cook).

Na kazi hiyo ilifanywa kwa kiasi kikubwa Kinda Olexandir Zinchenko akicheza kama beki anayeingia kwenye eneo la kiungo wakati city wakiwa na mpira (inverted full back). Mara nyingi alionekana kupiga mipira mirefu nyuma ya mabeki wa Bournemouth ili kumtafuta Leroy Sane na kuleta madhara kwa Bournemouth. Ndivyo lilivyopatikana goli la kwanza ambapo mpira ulipigwa na Zinchenko ukiwa unakimbiliwa na Sane, ulimshinda golikipa Asmir Begovic na kuupangua. Na ndio ulipoonekana ufundi mwingine wa Guardiola wa kuweka wachezaji kulizunguka boksi la wapinzani ili kushinda mipira ya Mara ya pili (second balls) kwani Bernando Silva aliuwahi na kufunga goli safi.

Bournemouth walionekana kuchachamaa baada ya hapo huku wakitupia vyema kqsi ndogo ya mabeki wa pembeni wa city (Danilo na Zinchenko) kwa kuwapata wakati wakiwa wameingia kwenye eneo la kiungo wao walishambulia kwa kushtukiza kutokea pembeni. Na kufanikiwa kupata goli dakika chache kabla ya mapumziko.

Ni wazi city walikosa ukakamavu (aggressiveness) katika kushinda mipira na kufanya pressing, kitu kilichowafanya cherries wacheze vyema, lakini Pep Guardiola kwa Mara nyingine akashinda, kwani kipindi cha pili city waliendelea kutawala mchezo zaidi, huku wakiwaingiza viungo washambuliaji wa pembeni (Raheem sterling na Leroy Sane) kwenye nafasi kati ya mistari ya ulinzi (half space) na mabeki wa pembeni has a upande wa kulia kwa Danilo, walianza kusogea mbele na kuongeza idadi ya watu kwenye eneo la kushambulia.

Dakika chache baadae Danilo alipiga mpira uliopangulia na Begovic na kisha Sterling akafunga goli lililofanana na la kwanza (second ball). Hii ni city katika ubora wake chini ya kocha Josep Guardiola ambaye kupitia kitabu cha Marti Pernanau-Pep confidential anatuonyesha moja kati ya nadharia inayopendwa na Guardiola kuwa: baada ya kufanya build up vizuri na kusogea katika eneo la mpinzani pep, anaitaka timu yake kujaribu kupiga mashuti na krosi zenye nguvu, kisha viungo washambuliaji walizunguke boksi la wapinzani kwa minajili ya kushinda second balls na kutoa mpira kimiani na ndio ilikuwa hukumu ya Bournemouth Leo hii second balls, second balls, second balls.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here