Home Kitaifa Nani wa KUIZUIA Yanga?

Nani wa KUIZUIA Yanga?

5963
0

Yanga imeshinda mechi ya 17 kati ya mechi 19 ilizocheza za ligi kuu Tanzania bara msimu huu. Ushindi wa 3-1 dhidi ya Mwadui unaendelea kuiongezea pointi katika nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa ligi.

Katika mechi 19 ambazo Yanga imecheza, haijapoteza mchezo hata mmoja. Imetoka sare michezo miwili na kushinda mingine 17, sasa imefikisha pointi 53.

Michezo 19 ni nusu ya mechi zote (38) za ligi msimu huu, ambapo hadi sasa Yanga ndio timu pekee ambayo haijapoteza mechi kwenye ligi.

Yanga imezipiga bao Azam na Simba ambazo ndio zinaweza kutoa changamoto kwenye kuwania ubingwa wa ligi msimu huu. Azam ina pointi 40 ikiwa imecheza mechi 17 (mechi mbili) nyuma ya Yanga wakati Simba yenyewe ina pointi 33 baada ya kucheza michezo 14 (michezo mitano) nyuma ya Yanga.

Endapo Azam na Simba zitashinda mechi zao zote za viporo na kuifikia Yanga idadi ya mechi ilizocheza (19) bado Yanga itaendelea kuwazidi pointi wapinzani wake kwenys mbio za ubingwa.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here