Home Kitaifa Mwigulu afunguka Singida United kupoteana ligi kuu

Mwigulu afunguka Singida United kupoteana ligi kuu

2186
0

Kiongozi wa Singida United Dr. Mwigulu Nchemba amesema kuondokewa na wachezaji wengi kwenye timu yao na mabadiliko kwenye benchi la ufundi kumepelekea kushindwa kupata usawa wa kiushindani katika ligi.

“Mwaka jana Singida ilikuwa na msimu mzuri, ilimaliza katika nafasi 5 za juu kwenye ligi ikafika hadi fainali ya kombe la TFF”-Dr. Mwigulu Nchemba.

“Wachezaji wengi waliokuwepo mwaka jana mwaka huu hawapo kwa sababu mbalimbali wengine wakiwa wamepata sehemu nyingine ambazo zinawanufaisha zaidi. Sasa hivi timu imeanza kujengwa upya, asa timu ikiwa inajengwa halafu ligi inaendelea madhara yake ndiyo ya namna hii.”

“Tunachofanya sasa hivi ni kuhakikisha timu inaendelea kuwepo kwenye ligi lakini jambo lingine kule ambako tunaweza kuwa bingwa tutapambana tuwe bingwa kwa sababu tupo kwenye robo fainali ya kombe la TFF.”

Singida United ipo nafasi ya 16 kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 33 baada ya kucheza mechi 28. Ijumaa March 15, 2019 ikiwa ugenini kucheza dhidi ya Azam FC kwenye uwanja wa Azam Complex ilichezea kisago cha bao 4-0.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here