Home Kimataifa Mtibwa sugar kipi kinawasibu msimu huu?

Mtibwa sugar kipi kinawasibu msimu huu?

3809
0

Makala na Raphael LucasKikosi cha wauza sukari kutoka kule manungu tuliani mjini Morogoro Leo kimeshuka uwanjani kuwakabili wana Ndanda kuchere kutoka Kwa walima korosho Mtwara na mchezo kuisha kwa sare tasa ya kutofungana na inakua mechi ya 20 kwa mtibwa huku wakishinda michezo 8 kupoteza 8 na sare 4 huku wakijikusanyia pointi 28 katika nafasi ya 7.Kikosi cha Mtibwa kinachonolewa na Mchezaji mkongwe wa wauza sukari Zuberi Katwila kimekua na matokeo yasiyo ya huu kulizisha msimu huu toka itolewe kwenye mashindano ya kimataifa ambapo imekua na panda shuka panda shuka nyingi kiasi kwamba kupoteza imani kwa mashabiki wake hasa walio zoea kuiona ikigombania nafasi 4 za juu huku msimu kutoenesha ushindani huo.Wakati mwingine najaribu kujiuliza ni wapi Mtibwa sukari wanakosea ikiwa wana wachezaji wazuri tu akina Stamili Mbonde, Kihimbwa, Kelvin Sabato na wengine wengi ambao ni wachezaji vijana wenye uwezo mkubwa.Msimu uliopita Wauza sukari hawa wa manungu walifanya vizuri sana na kupelekea kua mabingwa wa kombe la shirikisho Tanzania bara na kuwakilisha nchi kwenye mashindano ya kimataifa ambapo safari yao haikufika mbali baada ya kuishia pale Uganda kwa KCCA na kufurushwa nje ya mashindano hayoUnaweza ukafikili kua Mtibwa walitumia nguvu nyingi sana katika kuhakikisha wanakua mabingwa wa kombe la shirikisho ambayo inaweza kua chanzo cha wao kutokua na matokeo mazuri msimu huu pamoja na benchi la ufundi kutofanya vizuri.Ni mda mwafaka kwa kocha mkuu wa kikosi hicho Zuberi Katwila kufanya mabadiliko makubwa hasa kimfumo kwa wachezaji wake pamoja na kuongeza hamasa ili kuifanya timu kufanya vizuri vinginevyo timu itaendelea kutofanya vizuri na kupelekea kuhatarisha kibarua chake”Katwila shituka mapema kaka Mtibwa inapotea kwenye ushindani wake wa kati”Raphael Lucas (udom)0710690782/0764764449

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here