Home Kitaifa Mtibwa inakwama wapi?

Mtibwa inakwama wapi?

3048
0

Nikujuze tu kwa ufupi, Mtibwa Sugar haijashinda mchezo wowote wa ligi tangu tumeingia mwaka 2019!

Mtibwa imeshindwa kufanya vizuri kwenye ligi tangu ilipotolewa kwenye mashindano ya CAF Confederation Cup 2018/19. Mtibwa ilitolewa mwezi December 2018 kwa kufungwa michezo yote miwili (KCCA 3-0 Mtibwa Sugar, Mtibwa Sugar 1-2 KCCA).

Baada ya Mtibwa kutolewa kwenye mashindano ya kimataifa ikarudi kwenye ligi ambapo ilishinda 2-0 dhidi ya Azam FC ikiwa timu ya kwanza kuifunga Azam msimu huu, hiyo ilikuwa December 29, 2019.

Tangu iliposhinda mchezo wake wa ligi dhidi ya Azam, Mtibwa imecheza mechi 9 bila kushinda! Ni mwendo wa sare na vipigo. Tangu January 8, 2019 Mtibwa imepoteza mechi 6 na kuambulia sare 3.

Tanzania Prisons 2-0 Mtibwa Sugar
Mbeya City 1-0 Mtibwa Sugar
Mtibwa Sugar 0-1 Lipuli
JKT Tanzania 0-0 Mtibwa Sugar
Mtibwa Sugar 0-0 Ndanda
Mtibwa Sugar 1-1 African Lyon
Mwadui 1-0 Mtibwa Sugar
Biashara United 2-1 Mtibwa Sugar
KMC 1-0 Mtibwa Sugar
Mtibwa Sugar ?? Coastal Union

Mtibwa inakwama wapi? Inawachezaji wazoefu (Kado, Baba Ubaya, Dickson Daudi, Salum Kanoni, Nditi, Henry Joseph) wapo pia wachezaji vijana (Kihimbwa, Sabato, Rifat Semtawa, Dickson Job) wana benchi la ufundi zuri lenye likiongozwa na kocha Zubery Katwila na Mkurugenzi wa Ufundi Salum Mayanga.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here