Home Kimataifa Mtazamo wangu kuelekea mchezo wa United dhidi ya Liverpool

Mtazamo wangu kuelekea mchezo wa United dhidi ya Liverpool

5317
0

Manchester United wanakutana na Liverpool uwanjani Old Trafford siku ya Jumapili kwenye mchezo muhimu wa Ligi Kuu Uingereza.Liverpool wako juu ya Man United wakiwa na pointi 65, baada ya kucheza mechi 26. Man United wamecheza mechi sawa na Liverpool ila wao wako nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu.Ukiachilia mbali utamaduni wa Manchester United na Liverpool, ambao unaonekana kuwa mkubwa zaidi kwa Soka la Uingereza, mechi ya Jumapili ni muhimu sana kwa timu zote mbili.Ushindi kwa Liverpool, utaisidia kuwa na matumani ya Ubingwa na kuicha Man City kwa pointi tatu.Kwa upande mwingine, Man United pia wamesha moto chini ya Ole Gunnar Soskjaer. Watapambana wapate pointi tatu dhidi ya Liverpool ili waendelee kusogea kwenye nafasi za juu.Tuangalie mambo 4 ya kuzingatia kuelekea mechi yenyewe.1. Liverpool lazima wamzuie Pogba.Paul Pogba, yuko kwenye kiwango chake baada ya ujio wa Ole Gunnar Soskjaer. Mpaka sasa amefunga magoli 14, assists 8 kwenye mechi zote 32 msimu huu. Amepewa uhuru wa kushambulia, na ni hatari akiwa katika eneo la tatu na la mwisho wa uwanja.Beki wa Liverpool Virgil Van Djick atarejea, hivyo uwepo wake utamruhusu Fabinho kucheza kiungo mkabaji. Giorginio Wijnaldaum atapaswa kucheza badala ya Jordan Henderson kwasababu anapatikana karibu kila sehemu ya uwanja. Hivyo atashirikiana na Fabinho kumzuia Paul Pogba.2. Man United watahitaji kuongeza idadi ya wachezaji kwenye eneo la tatu na la mwisho wa uwanja.Kama Lingard na Martial watajumuishwa kwenye kikosi, watalazimika kutumia watu watatu mbele. Rashford, Martial na Lingard ili kuipa shida safu ya Ulinzi ya Liverpool.Endapo hawatahusika kwenye mchezo, Mata acheza kwenye 4-4-2 kusaidiana na Herrera, Pogba kuongeza ubunifu ili Rashford na Lukaku wasipate shida.3. Utatu wa Liverpool utatakiwa kuboresha kiwango.Mechi kadhaa, Sadio Mane, Firmino, Salah wameshindwa kucheza kwa ubora wao uliozoeleka. Pia wameshindwa kufunga hata goli moja dhidi ya Bayern kwenye mechi ya Uefa.Salah ambaye ana magoli 20 mpaka sasa, ameshindwa kufunga goli dhidi ya Vilabu vikubwa. Firmino yeye anakaba, amekuwa mzuri kwa mipira ya hewani na anaweza kufunga magoli ya vichwa.Victor Linderof na Baily, lazima wawe makini kutokana na umahili wa Salah mwenye uwezo kuingia ndani ya uwanja akiwa na mpira. Luke shaw na Young watakuwa na wakati mgumu hasa pale mabeki wa pembeni wa Liverpool watakapokuwa wanawasaidia Mane na Salah kuongeza presha.4. Kumiliki mpira itakuwa muhimu zaidi kwenye eneo la kiungoNemanja Matic na Fabinho, hawataweza kuvuka nusu yao ya uwanja. Watabaki kwenye sehemu yao muhimu ya kulinda. Keita atahitaji kuonyesha umahili wake maana amekuwa akifananishwa na Pogba kiuchezaji.Pogba na Herrera, watakuwa na kazi kubwa ya kuifanya United imiliki mpira pamoja na kusaidia kutengeneza mashambulizi. Naona Adam Lallana atahusishwa kwasababu ya kutuliza mchezo pamoja na kumliki mpira. Kiungo huyo ambaye amefunga magoli 21 kwenye mechi zake 151 kwa Liverpool, uzoefu wake unaweza kutumika kwenye mechi hiyo.Na Patrick Admila

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here