Home Kimataifa Mtazamo wangu juu ya Jorginho ndani ya klabu ya Chelsea.

Mtazamo wangu juu ya Jorginho ndani ya klabu ya Chelsea.

4672
0

Kila kukicha kwa wale wanafiatulia wa mchezo wa soka habari ya mjini ni muendelezo mbovu wa kocha wa klabu ya Chelsea, Maurizio Sarri ,na kiungo wa klabu hiyo Jorginho, kutofanya vizuri katika ya kiungo nini tatizo kubwa?Jorginho, ni moja ya wachezaji wazuri katika ligi kuu England anasifika kwenye umiliki wa mpira na kupiga pasi fupi fupi ukimuangalia kabla ya kuja Chelsea,akitokea Napoli, msimu uliopita ndo alikuwa mchezaji anayeongoza kupiga pasi nyingi katika ligi kuu tano bora Barani Ulaya wapo watakosema ligi hiyo ni nyepesi ila ligi kuu Itali ni moja ya ligi bora duniani.Katika ligi kuu England , unahitaji kiungo mkabaji mwenye uwezo mkubwa wa kukaba ,kukimbia na kupora mipira katika idara hiyo ukiangalia Chelsea hilo ndo tatizo lao kubwa.Jorginho katika idara hiyo ni mzito kwenye kukaba na hata kukimbia hii inapelekea kuonekana Chelsea katika idara ya kiungo mkabaji inapwaya na watu kutumia kama mwanya wa kupitia na kupata matokeo huwa tunaamini timu bora lazima idara ya kiungo ikamilike kwa sababu ndo muunganiko wa timu inapoanzia haswa mfumo wa timu ambayo inataka kumiliki mpira kwa mda mrefu.Kiukweli Sarri, anahitaji amrudishe Kante katika idara hiyo kwa sababu Kante ana uwezo wa kukaba kukimbia na hata kupora mipira ukiangalia makocha wa hivi karibuni wamepita Chelsea wamepata mafanikio kwa kumtumia Kante kiungo wa kati mkabaji.Mfano mzuri ukiangalia Manchester City, katika idara ya kiungo mkabaji Fernandinho,anakaba kukimbia na hata kupora mipira kwenye idara hiyo.Timu nyingi kwa sasa katika ligi kuu England sijajua udhaifu wa Chelsea kuwa Jorginho, ukienda kufanya press kwake ni rahisi sana kuchukua mipira au kumpa presha na kupoteza mpira.Katika ligi kuu England ukifuatilia wachezaji wanaocheza katika idara viungo wakabaji wana nguvu sana mfano mzuri angalia Leicester City Ndindi, Tottenahm Wanyama, Manchester United , Matic .Azizi Mtambo 15

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here