Home Kimataifa Msuva aiokoa timu yake nyumbani

Msuva aiokoa timu yake nyumbani

3630
0

Simon Msuva jana ameiokoa klabu yake Difaa El Jadida kuchezea kichapo dhidi ya RSB Berkane kwenye uwanja wa nyumbani baada ya kuisawazishia bao kwenye mchezo wa ligi (Botola Pro) uliomalizika kwa sare ya 1-1.

Berkane walitangulia kupata bao dakika ya pili kupitia kwa Mohamed Aziz lakini Msuva akasawazisha mzani dakika ya 67.

Hadi sasa Difaa El Jadida ipo nafasi ya 11 kwenye msimamo wa ligi yenye timu 16 ikiwa na pointi 21 baada ya kucheza mechi 18. El Jadida imeshinda mechi 5, sare 6 na vipigo 7.

Raja Casablanca inaongoza ligi ikiwa na pointi 36 baada ya kucheza mechi 18.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here