Home Kimataifa Msimu Mpya Wa NBA Waanza, Vita Ya Kyrie Irving Dhidi Ya Lebron...

Msimu Mpya Wa NBA Waanza, Vita Ya Kyrie Irving Dhidi Ya Lebron James Yaingia Dosari.

4326
0
Boston Celtics' Kyrie Irving, right, drives past Cleveland Cavaliers' Iman Shumpert in the first half of an NBA basketball game, Tuesday, Oct. 17, 2017, in Cleveland. (AP Photo/Tony Dejak)

Baada ya kusubiri kwa muda mrefu tangu Golden State Warriors wawe mabingwa wa msimu wa 2016-2017 hatimaye msimu mpya wa 2017-2018 umeanza rasmi alfajiri ya leo huku kukiwa na drama za hapa na hapa hasa kutokana na usajili wa msimu huu ulivyofanyika.

Tofauti na ilivyotegemewa na wengi, msimu huu Kyrie Irving alikuwa ndiye mchezaji wa kwanza kutangaza hadharani nia yake ya kutotaka kucheza na Lebron James na kuhitaji kwenda kwenye klabu nyingine ambapo timu iliyokuwa inaweza kutoa walichohitaji Cavaliers ikawa ni Boston Celtics kwa kuwatoa Jae Crowder na Isaiah Thomas.

Ukiwa na mchezo ambao ulitegemewa kuvuta hisia za wengi hasa kuongeza wigo wa watazamaji, Kyrie Irving kama ilivyotegemewa alizomewa kila pale ambapo aligusa mpira ndani ya uwanja wa Quicken Loans Arena, Ohio Cleveland. Lakini hisia za upinzani huu hazikudumu sana kwani mchezaji Gordon Hayward ambaye naye alikuwa mchezaji aliyesajiliwa na Boston Celtics alitua vibaya wakati akiruka na kupelekea kuvunjika mguu wake kwenye maeneo ya mfupa wa ugoko na kutengua Kifundo cha mguu.

Majeruhi haya yanayoweza kumweka nje kwa msimu huu wote yalipelekea mchezo kubadilika huku wachezaji wote wakionekana kuumizwa na tukio hilo lakini Cavaliers waliweza kuibuka na ushindi wa pointi 102-99. Lebron James alifunga pointi 29, Kevin Love akaongeza 15 na Derick Rose akafunga 14 kwa upande waCavs.

Kyrie Irving alimaliza mchezo na alama 22 na assist 10 huku mchezaji Jaylen Brown aliyeibuka na kuziba nafasi ya Hayward ndani ya mchezo akimaliza mchezo huo na alama 25.

HIGHLIGHTS

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here