Home Ligi BUNDESLIGA Mourinho Vs Guardiola nani kiboko kwa kumwaga mikwaja: Wametumia zaidi ya trillioni...

Mourinho Vs Guardiola nani kiboko kwa kumwaga mikwaja: Wametumia zaidi ya trillioni 5 kwenye usajili

9706
0

Kwa kipindi cha miaka 10 iliyopita, soka barani ulaya limeendelea kuwa biashara kubwa. Wachezaji wamekuwa wakiuzwa na kununuliwa kwa mabilioni ya pesa kutoka timu moja kwenda timu nyingine, ndani ya ligi moja au ligi za nchi tofauti.

Katika kipindi cha miezi miwili hii ya dirisha la usajili klabu kama Manchester City tayari imetumia takribani £205m sawa na zaidi ya billioni 600 za kitanzania kusajili wachezaji wapya, huku wapinzani wao Man United wakitumia £105 takribani billioni 300 kuimarisha kikosi chao.

Vikosi hivi vinaongozwa na moja ya makocha ambao katika kipindi cha miaka 10 iliyopita wametumia fedha nyingi zaidi katika kuimarisha timu zao walizozifundisha kwa wakati huu; Pep Guardiola na Jose Mourinho.

Mhispaniola Pep ameripotiwa kutumia jumla ya paundi million 899 kusajili wachezaji katika vilabu vya FC Barcelona, Bayern Munich na sasa City. Fedha hizi ni zaidi ya Trillioni 2.5 za kitanzania, Pep ametumia ndani ya miaka 10 kufanya usajili

Pep kwa dirisha hili la usajili amevunja rekodi ya matumizi makubwa zaidi kwa dirisha moja la usajili kwa kutumia zaidi ya £205 na huenda bado hajamaliza usajili. Usajili wa beki Benjamin Mendy umeweka rekodi ya kuwa ghali zaidi katika historia ya soka, alitumia £52m kumsaini beki huyo wa Ufaransa kutoka Monaco.

Safu ya kiungo pekee ya Manchester City ambayo iliundwa na usajili wa Pep kutokea msimu wake wa kwanza mpaka sasa imetumia kiasi cha £227m.

  • Benjamin Mendy £52m
  • Kyle Walker £50m
  • John Stones £47.5m
  • Ederson £35
  • Danilo £26m
  • Bravo £17m

Pep alipoanza kazi Barcelona mpaka anamaliza alitumia jumla ya kiasi cha paundi millioni 285 ndani ya misimu 4 aliyoifundisha pale Camp Nou.

Mwaka uliofuatia alipumzika kazi, kisha msimu uliofuatia akaelekea Allianz Arena kuifundisha FC Bayern Munich.

Alikaa Bayern Munich kwa miaka 3 na kabla ya kuelekea Etihad Stadium, alikuwa ameshatumia jumla ya paundi millioni 185.

Jose Mourinho kwa upande amefundisha vilabu vya Real Madrid, Chelsea na Manchester United.

Alianza kazi yake ndani ya Manchester United kwa kufanya usajili uliogharimu kiasi cha £146m – akiwasaini Eric Bailly, Henrikh Mhikitaryan na kisha akavunja rekodi kwa kumsaini Paul Pogba kwa £89m.

Msimu huu Mourinho alianza kwa kumsaini Lindelof na kisha akamsaini Lukaku, kwa mujibu wake anasema bado anahitaji wachezaji wawili kabla ya dirisha la usajili kufungwa mnamo September 2.

Kwa ujumla katika kipindi cha miaka 10 iliyopita ametumia takribani paundi millioni 846 kwenye kufanya usajili. Akiwa Inter Milan ambapo alitumia jumla ya £136m kwa misimu miwili aliyokaa Guiseppe De Meazza.

Real Madrid alitumia kiasi cha £159m katika misimu 3 aliyokaa katika klabu hiyo yenye maskani yake Santiago Bernabeu.

Awamu yake ya pili ndani ya Chelsea ilianza kwa Mourinho kutumia £108m msimu wa kwanza na kisha £116m msimu wa pili, kisha msimu wa 3 akatumia £74m. Mpaka anatimuliwa alikuwa ameshatumia kiasi cha £298m.

******************************************************************

Mpaka sasa makocha hawa wawili wameshatumia takribani paundi billioni 1.8 – Ukileta kwenye fedha za madafu fedha hizi zinakaribia kufikia trillioni 5.2. Fedha hizi pekee zingetosha kuinunua klabu ya Arsenal yenye thamani ya billioni 2.02 za kitanzania.

*Soka ni moja ya biashara kubwa duniani*

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here