Home Ligi EPL “Mourinho mmoja sura tofauti”-Shaffih Dauda

“Mourinho mmoja sura tofauti”-Shaffih Dauda

3963
0

Mourinho wa mwanzoni mwa miaka ya 2000, Mourinho wa Inter na Real Madrid na Mourinho aliyerudi Chelsea kwa mara ya pili na baadaye Manchester United ni Mourinho wa version tatu tofauti.

Mourinho wa kwanza ni yule aliyekuwa na njaa na anatamani awe mtu fulani kwa hiyo namna alivyokuwa anafanya kazi kulikuwa na kitu kinachompa motisha ya kupata mafanikio.

Mourinho wa pili ni yule ambaye alikuwa anapata mafanikio lakini alikuwa anataka kuthibitisha kwamba hajabahatisha na anataka kutengeneza historia miongoni mwa makocha bora kuwahi kutokea katika kipindi fulani.

Mourinho wa tatu ni yule ambaye ameshamaliza kila kitu hana cha kupoteza kwa hiyo hana presha na ndio maana anakuwa jeuri na mwisho wa siku anaishia kugombana na wachezaji.

Zidane ameshavuka stage ya kwanza ya Mourinho yupo kwenye stage ya pili ya kutaka kuuthibitishia ulimwengu kwamba aliyoyafanya akiwa Madrid hakubahatisha.

Kwa upande wa Guardiola yeye yupo kwenye level moja na Mourinho lakini anataka kuandika historia kwenye klabu ya Man City ambayo ni project na yeye awe sehemu ya mafanikio ya hiyo project.

Ukifatilia baada ya mechi ya Liverpool vs Manchester United weekend iliyopita, Mourinho aliwasifu baadhi ya wachezaji wa Liverpool lakini akawatukana wachezaji wake badala ya kuweka muda wa kuwajenga wachezaji wake kama Lukaku ili wafunge magoli na kujiamini.

Wachezaji wakifanya vizuri wanazungumzwa vizuri kwenye vyombo vya habari, timu itauza jezi nyingi za wachezaji wanaofanya vizuri sasa leo ni mchezaji gani wa Man United ambaye watu wanataka kuandika jina lake kwenye jezi, Mourinho amefeli ndio maana ameondoka.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here