Home Uncategorized Moto mkali watetekeza maisha ya chipukizi wa klabu ya Flamengo

Moto mkali watetekeza maisha ya chipukizi wa klabu ya Flamengo

2900
0

Moto uliozuka katika uwanja wa mazoezi karibia na kambi ya vijana wa klabu ya Flamengo umeua watu kumi.

Kambi hiyo ya kulelea vijana wadogo maarufu kama Ninho de Urubu ipo karibu na sehemu ya malazi ya watoto wadogo.

Taarifa zinaeleza kuwa uwezekano mkubwa wa watu hao kumi waliopoteza maisha ni vijana hao chipukizi. Zimamoto walifika katika eneo hilo lakini moto ulishasambaa eneo kubwa.

Kinda wa Real Madrid Vinicious Junior ambaye pia alilelewa katika kambi hiyo alituma ujumbe wake kwenye ukarasa wa Twitter akiwaombea wahanga wa tukio hilo. Kambi hiyo ilifanyiwa marekebisho miezi miwili iliyopita

Msemaji wa klabu hiyo amethibitisha kuwa moto huo ulitokea saa 5 usiku watoto wakiwa wamelala. Hakuna taarifa ya chanzo cha moto huo. Watu wengine wanne walijeruhiwa vibaya sana na moto huo.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here