Home Kimataifa Morata mbele ya Pilato Simeoni

Morata mbele ya Pilato Simeoni

3061
0

Wastani wa Alvarato Morata kufunga akiwa katika uzi wa Chelsea ni asilimia 0.333 kwa kila mechi, akiwa ameitumikia Chelsea kwa zaidi ya mechi 72……….Morata amefunga magoli ishirini na nne tu idadi ndogo sana hasa ukilinganisha na eneo analocheza kama mshambuliaji wa mwisho katika timu……….Idadi hiyo angefunga Marcos Alonso isingekuwa ishu sana angesifiwa maana so kazi yake ila kwa morata aliletwa chelsea kwa kazi moja tu nayo kufunga kila akiamka alitakiwa kuwaza lango la timu pinzani……….Kichwani kwake alitakiwa kuwaza kama Didier Drogba lakini haikuwa hivyo kwa Morata.………Alionekana kama amefunga baraka za magoli ndani ya chelsea kwani kwa chelsea chini ya morata wametengeneza jumla ya magoli sitini na mbili kwa msimu wa 2016/17,wakati kwa msimu wa nyuma yake walifunga magoli 85…………Alikuja kama mrithi wa mtukutu diego costa rekodi zake akiwa klabu ya juventus zilionesha ana kitu ila alihitaji kupewa muda, wakampa muda lakini akabaki kuwa Morata yule yule……….Ameondoka klabuni kumpisha mshambuliaji Gonzalo higuain amekwenda kuitumikia Atletico Madrid kwa mkopo wa mwaka mmoja na nusu. Huko anaenda sehemu sahihi ambayo kwa falsafa yao katika kuwafundisha washambuliaji imeonekana kuwa na matunda chanya.………Watu kama Radamel Falcao, Sergio Aguero, Diego Costa bila kumsahau El Nino mvua ya magoli Fernando Torres. Wote walipita Vincente Calderon. Hawa ni matunda ya kazi nzuri ya Diego Simeone na benchi lake la ufundi……….Morata anarudi nyumbani alipoanza kucheza soka lake katika klabu hiyo. Naamini anafahamu nini kinahitajika pale. Morata anapaswa kupaki gari yake ya audi nyumbani kwake na kwenda mazoezi na akili ya kufunga……….Kwa mshambuliaji wa Atletico kila mechi anatakiwa acheze kama fainali. Apigane kwa kila hali hata uchizi wa Diego Costa umechangiwa kwa kiasi kikubwa na malezi ya Atletico. Kwao mpira ni vita, ni mapambano ya dakika 90 kwa ajili ya ushindi.………Kwa macho ya mbali morata amekwenda sehemu sahihi sehemu ambayo atatukanwa, atapewa kejeli ili mradi tu afunge kwani kwa kipindi cha karibuni morata ameonekana kukosa kujiamini akiwa langoni……….Anaenda kukutana na Simeone mtu anatayempenda tu kama akiwa anafunga, malezi ya kudeka ya antonio conte sidhani kama atayapata kwa el cholo huyu tunayemfahamu.Mwandishi MESHACK MELELE

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here