Home Uncategorized Mo Salah amuombea Aboutrika msamaha kwa Raisi

Mo Salah amuombea Aboutrika msamaha kwa Raisi

6148
0

☰Egypt

Mohamed Salah amemuombea msamaha Aboutrika kwa raisi akiomba aruhusiwe kuingia tena nchini huko.

Nyota huyo wa Egypt na Liverpool amemuomba raisi Abdel Fattah Al-Sisi kumruhusu nyota wa zamani wa Al Ahly na timu ya taifa Mohamed Aboutrika radhi.

Kwa mujibu wa Al-Khaleej Al-Jadeed, Salah alijaribu kuongea na baadhi ya viongozi wa nchini humo kumuombea radhi Abou.

Abou alishukiwa na serikali ya nchi hiyo kwa madai kuwa alijihusisha na kikundi cha kigaidi cha Muslim Brotherhood, ambacho kilisababisha machafuko nchini humo.

Salah anaamini kuwa Abou Trika ana msaada kwenye timu ya taifa kwenye michuano ya AFCON.

Abou ambaye anashikilia rekodi ya kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa afrika mara 4 amekuwa akiishi nje ya Misri kwa muda wa miaka miwili.

Abou anakumbukwa na bao lake la mwisho ambalo alilofunga mwaka 2008. Abou alistaafu soka mwaka 2013 mara baada ya klabu yake kufungwa katika michuano ya klabu bingwa ya dunia.

Abou amewahi pia kufanya matukio mbalimbali ya kusaidia wahitaji. Mwaka 2005 alicheza kikosi cha pamoja na zidane na Delima kwenye mchezo uliondaliwa na UNDP kusaidia wahitaji.

Amekuwa balozi mzuri sana ndani ya taifa lake licha ya kukumbwa na kashfa hiyo kubwa.

Maombi ya Mo Salah pia yanatarajiwa kupewa shavu na raisi wa shirikisho la soka nchini humo bwana Hany Abu Rida.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here