Home Kimataifa Mnajadili offside za Higuani mnaacha kumjadili Zapata!? Hizi dharau mnatoa wapi?

Mnajadili offside za Higuani mnaacha kumjadili Zapata!? Hizi dharau mnatoa wapi?

5295
0

………Katika ligi kuu ya Seria A kuna huyu mtu anajulikana kama Duvan Zapata raia wa Colombia. Anacheza nafasi ya Straika nafasi ambayo timu nyingi ulimwenguni zinahangaika kupata mtu makini kama mimi enzi zangu. Ana miaka 27 na amejiunga na klabu ya Atlanta akitokea klabu ya Sampdoria kwa mkopo.

………Yaweza kuwa sio jina geni sana katika masikio ya wale mashabiki wa ligi ya Seria A maana aliwahi kucheza Napoli tangu mwaka 2013 – 2018. Napoli mambo hayakwenda sawa sana. Alifanikiwa kufunga mabao 11 tuu akiwa Napoli.


Alipokuwa Napoli mwaka 2015-2017 alipelekwa katika Klabu ya Udinese kwa mkopo ambako alifanikiwa kuifungia klabu hiyo magoli 18 katika michezo 63.


………Mwaka 2017- 2018 klabu ya Sampdoria walimsajili kwa mkopo kukiwa na kipengele cha kumsajili moja kwa moja. Alicheza mechi 31 huku akipasia nyavu mara 11 . Kisha baada ya kurishishwa na miwangonchake wakamsajili moja kwa moja kisha wakamtoa kwa mkopo kwenda Atlanta msimu wa 2018/2019.

………Ndani ya Atalanta katika mechi 21 alizocheza ametia kambani mabao 17. Wachache sana wameandika kuhusu yeye. Labda upepo wa New Man United au ujio wa Higuain umeondoa kurasa za yeye kuandikwa. Amekuwa na rekodi murua sana tokea tare 3 mwezi Disemba amefunga magoli 17 katika michezo 10.

………Jana usiku Atalanta waliwakalibisha Juventus katka kombe la Coppa Italia ambapo ilishudiwa juventus akikalishwa goli 3 kwa bila.………Aliweza kufunga goli mbili katika mechi hiyo na kuihakikishia ushindi timu yake katika usiku wa jana. Katika msimamo wa Ufungaji wa ligi ya Seria A yupo nafasi ya 3 akiwa na magoli 15 akiwa amefungamana na C. Ronaldo aliye nafasi ya pili.

………Tunamkosea heshima Zapata kama tutajadili offside za Higuain na kuacha kumjadili yeyem

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here