Home Kitaifa Mkongwe Simba atoa ushauri kuiangamiza Vita

Mkongwe Simba atoa ushauri kuiangamiza Vita

3052
0
Winga wa Simba SC, Steven Mapunda ‘Garrincha’ (kushoto) enzi zake akimtoka beki wa Malindi FC ya Zanzibar, Abdallah Ali katika mchezo wa Ligi Kuu ya Muungano (Picha na Bin Zubeiry Sports Online)

Mchezaji wa zamani wa Simba Steven Mapunda maarufu kama Garincha amezungumzia mchezo wa leo wa Simba vs AS Vita wa ligi ya mabingwa Afrika hatua ya makundi.

“Mchezo utakuwa mgumu sana kwa Simba kwa sababu wale jamaa (AS Vita) wamekuja wanataka ushindi na yeyote atakaeshinda anaingia robo fainali kwa hiyo Simba wajiandae wakijua mchezo huu utakuwa mgumu sana.”

“Ili waweze kushinda, viongozi wao inabidi wajiandae na wachezaji waandaliwe kisaikolojia. Najua wamejiandaa lakini wajue mchezo utakuwa mgumu.”

“Kwa uzoefu wangu, najua AS Vita ni wazoefu wa miaka mingi, mchezo wa kwanza wameshatuona na walitufunga goli 5-0 lakini hapa watataka ushindi japo wa goli moja tu waingie robo fainali.”

“Simba sio timu mbaya kama wakijipanga vizuri wanaweza kushinda mchezo huu.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here