Home Kimataifa Mkoa wa Meru waanda donge nono kutwaa klabu ligi kuu

Mkoa wa Meru waanda donge nono kutwaa klabu ligi kuu

3421
0

Serikali ya mkoa wa Meru wapo kwenye mazungumzo ya mwishoni na uongozi wa klabu ya THIKA UNITED ili kuinunua timu hiyo na endapo dili hilo litakamilika timu hiyo itabadilishwa jina na kuitaitwa MERU UNITED


Mwenyekitii wa michezo wa mkoa wa Meru bwana DANIEL KIOGORA uongozi wa Thika wamekubali dili hilo na wapo kwenye hatua za mwisho kuikamilisha. Aliongeza pia hadi kufika mwezi wa tatu mambo yote yatakua tayari.

Aliwahakikishia pia wana Meru kuwa dili hilo likikamilika basi wachezaji na benchi la ufundi itapitiwa upya mikataba yao na watasaini upya. Ameahidi kuwa wachezaji na maofisa wa klabu hiyo watalipwa stahiki zao na serikali ya mkoa wa Meru.
Mpaka sasa mkoa huo upo kwenye mchakato wa kujenga uwanja mpya utakaoingiza watu 25,000 kufikia mwishoni mwa mwezi wa pili.


THIKA UNITED wanaoshiriki ligi daraja la kwanza nchini Kenya wapo kwenye nafasi ya 14 baada ya mechi tisa. Hata hivyo maofisa wa Mkoa wa Meru imeandaa donge nono kwa ajili ya kuinua na kunoa vijana wenye vipaji.

Mkoa wa Meru haina timu inayoshiriki ligi kuu tokea mwaka 1990. Klabu ya mwisho kuwamo ligi ilikuwa timu ya MAFUKO BOMBERS ambayo ilishindwa kusalia ligi kuu.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here