Home Kimataifa Mishahara ya wachezaji gumzo Cameroon

Mishahara ya wachezaji gumzo Cameroon

3756
0

Inaelezwa zaidi ya asilimia 70 ya vilabu kwenye madaraja ya ligi mbili za juu nchini Cameroon havijalipa mishahara wachezaji wake kwa zaidi ya miezi sita.

Mchezaji wa zamani wa Cameroon Geremi Njitap ambaye ni kiongozi wa umoja wa wachezaji nchini humo alisema vilabu 24 kati 33 vimeshindwa kufikia makubaliano ya malipo na wachezaji kinyume na makubaliano ya kimikataba.

Njitap ambaye ni mchezaji wa zamani wa Chelsea na Real Madrid amesema, wachezaji wengi wanaishi maisha magumu kufuatia timu zao kushindwa kuwalipa mishahara na ‘marupurupu’ kwa miezi kadhaa.

FIFA wameingilia kati na wamelitaka shirikisho la soka nchini Cameroon (FECAFOOT) lifanye uchunguzi na kuhakikisha kwamba wachezaji wanalipwa stahiki zao au Cameroon inaweza kukutana na adhabu ambayo ni pamoja na ligi kusimama hadi pale stahiki za wachezaji zitakapolipwa na kutakuwa na uhakika wa mustakabali wa muda mrefu wa wachezaji kulipwa kulingana na mikataba.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here