Home Ligi BUNDESLIGA Miroslav Klose aamua kuvua viatu na jezi.

Miroslav Klose aamua kuvua viatu na jezi.

1228
0

a-espncdn-com

Moja ya wachezaji bora kuwahi kutokea nchini Ujerumani, Miroslav Klose ametangaza kuachana rasmi na soka kama mchezaji na sasa anatazamia kujiunga na benchi la ufundi la timu ya Taifa ili awe moja ya makocha.

Klose, ambaye alistaafu kuchezea timu Taifa baada ya kutwaa kombe la Dunia mwaka 2014 , hakuwa na klabu yoyote tangu alipoamua kuachana na klabu ya Lazio katika majira yaliyopita ya kiangazi.

Mchezaji huyu mwenye umri wa miaka 38, ambaye pia alivichezea vilabu vya FC Homberg, Kaiserslautern, Werder Bremen na Bayern Munich, anabakia kuwa mchezaji aliyefunga magoli mengi zaidi katika jezi za timu ya Taifa ya Ujerumani akiwa na mabao 71 katika michezo 137 aliyoichezea.

Klose, akiwa ni moja ya wachezaji pia wenye mafanikio makubwa katika soka la Ujerumani, pia ni mchezaji mwenye magoli mengi zaidi kwenye fainali za kombe la dunia akiwa amefunga mabao 16 katika michuano hiyo.

“Nimepata ,afanikio mengi na makubwa nikiwa na timu ya Taifa,” Klose alisema kupitia tovuti rasmi ya chama cha soka Ujerumani,l DFB . “Ulikuwa ni wakati bora na usiosahaulika. Hii ndio sabbau nina furaha kurejea kufanya kazi na chama chetu cha DFB. Kwa miezi kadhaa iliyopita nilikuwa nafikiria kubaki uwanjani, lakini baada ya kuwaza juu ya mambo mengine wazo la kuwa kocha likanijia.”

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here