Home Kimataifa Michael Owen atabiri bingwa wa UEFA

Michael Owen atabiri bingwa wa UEFA

9205
0

Tokea mwaka 2012/13 hakuna timu nyingine zaidi ya Madrid ya na Barcelona zilizotwaa ubingwa wa klabu bingwa. Kwa kipindi kirefu vilabu vya England vimekuwa underdogs kwenye michuano hii kabla ya Liverpool kutinga fainali hizo mwaka jana.

Kwa sasa Madrid ambao wamekuwa wasumbufu wakubwa hawapo tena. Mabingwa hao wa jiji la Madrid walitwaa makombe 4 kati ya 5 chini ya kocha wao Zinedine Zidane ambaye amerejea tena.

Msimu huu ligi kuu ya England imeng’ara sana katika michuano hiyo. Timi zote zimepita kwa kishindo mara baada ya kushinda mechi za ugenini. Wow!

Matokeo hayo yanaamsha tena chachu ya kulisaka kombe hilo kubwa barani ulaya. Michael Owen anasema itakuwa fedheha kubwa kama timu 4 kati ya 8 zitashindwa kunyakuwa taji hilo.

Nyota huyo wa zamani wa Liverpool, Man United na Real Madrid anaamini huu ni mwaka wa England. Anaamini kwa asilimia 99 UCL inakwenda England.

Owen ametabiri kuwa kati ya Liverpool na Man City ya Mh Pep Guardiola lazima mmoja wao atwae ubingwa au hata wote kucheza fainali.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here