Home Kimataifa MEZA YA MAKUMBUSHO: Xavi pengo kubwa ndani ya Barcelona

MEZA YA MAKUMBUSHO: Xavi pengo kubwa ndani ya Barcelona

3668
0

BARCELONA, Hispania.
Xavier Hernandez ameondoka Katalunya. Hakuna tena mtu kama huyu dimba la kati. Kila kukicha wanahaha kumoata mrithi wake. Ivan Rakitic ni mzuri sawa lakini Xavi ni moja ya Kiungo bora duniani aliyewahi kufanya makubwa zaidi katika historia ya mchezo wa soka.

Tumesikia Barcelona inamfukuzia Rabiot lakini sina imani kama anaweza kuziba pengo lake.

Kiungo huyo, alikuwa akicheza eneo la Kiungo wa kati na uwezo mkubwa wa kumiliki wa mpira. Silaha yake kubwa ni kupiga pasi fupi fupi, kwa staili ya tik-tak.


Wanaompuuza Messi siku akistaafu soka ndio wataona umuhimu na ubora wake” Xavi


Wasifu wake

Hernandez, amezaliwa mwaka 1980, mwezi Januari. Kwa sasa ana umri wa miaka 39. Ni mzaliwa wa Hispania.

Historia yake kwa Ufupi

Mchezaji huyo ameanzia kucheza soka akiwa katika academic ya La Masia, mjijini Barcelona, akiwa na umri wa miaka 11 mchezo wake wa Kwanza kuchezea ilikuwa mwaka 1998 dhidi ya Mallorca. Baada ya hapo ameichezea Barcelona, jumla ya michezo 700 na kufunga mabao 85 na kutoa assist 60.

Xavi ameitumikia Timu ya Taifa ya Spain, kuanzia mwaka 2000 – 2014 michezo 133 na kufunga mabao 13.


Nadhani Kimichi atawafaa zaidi Barcelona” Xavi


Mafanikio

Mwaka 2010 alitwaa kombe la dunia nchini South Afrika. Mwaka 2008 na mwaka 2012 alitwaa kombe la Mataifa la Ulaya akiwa na Spain.


Baada ya fainali za mwaka 2014 kombe la dunia Kiungo huyo alitangaza kustafuu soka la kimataifa.

Xavi, akiwa na klabu ya Barcelona, ametwaa makombe 31 akiwa na Barcelona, na Timu ya Taifa ya Spain kombe la ligi kuu Spain, ametwaa mara 8 na kombe la Uefa ametwaa mara 4.

Xavi pia alitajwa kwenye kinganyiro cha wachezaji wa tatu kuwania tuzo ya Ballon d’Or 2010, na 2011.


Arthur Melo ni moja kati ya viungo wanaotajwa sana kutembea kwenye viatu vya Xavi. Kwenye mchezo wao wa ugenini dhidi ya Valencia, Melo alipiga pasi zilizokamilika 142, mara ya mwisho mchezaji aliyepiga pasi nyingi kwenye mechi ya ugenini zaidi ya 142 ni Xavi Hernandez vs Levante Nov 2012 (148).

Moja ya mafanikio makubwa binafsi ya Xavi ni kutajwa kwenye kikosi bora cha michuano ya Uefa mara tano 2008, 2009, 2010, 2011, na mwaka 2012.

Pia aliingia kwenye kikosi bora cha dunia mara 6 , 2008, 2009, 2010, 2012, na mwaka 2013.

Kwa mafanikio ya Xavi ni ngumu sana kupata mtu ambaye moja kwa moja anaweza kufikia kiwango hicho kirahisi. Wapo wachezaji wengi wenye uwezo lakini bado kufikia safari ya mafanikio yake inahitaji muda.

Azizi _Mtambo 15

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here