Home Kimataifa MEZA YA MAKUMBUSHO: Unamkumbuka Trazeguet

MEZA YA MAKUMBUSHO: Unamkumbuka Trazeguet

4343
0

David Sergio Trezquet, amezaliwa mwaka 1977 nchini Ufaransa, akiwa na umri wa miaka 42 pia amewahi kuitumikia timu ya taifa Ufaransa, alikuwa akicheza nafasi ya mshambuliaji.

Mshambuliaji huyo alianzia maisha ya soka nchini Argentina, katika klabu ya Atletico Platense, akiwa na umri wa miaka 8 baadaye mwaka 1994 alipandishwa katika klabu kubwa na kucheza ligi kuu ya Argentina.

Baada ya kuitumikia klabu hiyo Msimu unaofuata alihama na kwenda na kujiunga na Monaco, inayoshiriki ligi kuu Ufaransa, alikutana na mshambuliaji mwenzake Thienry Henry, msimu wa mwaka 1996-97 walitwaa kombe la ligi kuu Ufaransa.

Kabla ya kuondoka Monaco, aliifungia klabu hiyo mabao 52 katika michezo 93 ya ligi kuu pia alitwaa makombe mawili ya ligi kuu na kombe la Trophee des champion (kombe la ligi).

Msimu wa mwaka 2000 alijiunga na klabu ya Juventus, kwa ada ya uhamisho wa Euro milioni 20 msimu wa mwaka 2000-01 alichukua tuzo ya mfungaji bora alifunga mabao 24 na kutwaa taji la ligi kuu Itali.

Trezguet, ameifungia Juventus, Mabao 138 katika michezo 245 katika michuano yote na akiwa mchezaji wa nne kufunga mabao mengi katika historia ya Juventus.

Nyota huyo kwa ngazi ya taifa ameifungia mabao 34 katika michezo 71 akiwa na Ufaransa, kuanzia mwaka 1998-2008, ameichezea timu ya taifa ya Ufaransa, chini ya umri wa miaka 18,20,21.

Mwaka 2000 kwenye michuano ya kombe la Mataifa nyota huyo aliifungia Ufaransa, bao la ushindi dhidi ya Itali, alikuwemo kwenye michuano ya kombe la dunia 2002 michuano ya kombe la Mataifa 2004 pia ikumbukwe mwaka 2006 kwenye fainali za kombe la dunia alikosa penalt dhidi ya Itali.

Mwaka 2004 Shirikisho la soka duniani FIFA walikuwa wanasherekea miaka 100 tangu kuanzishwa FIFA, walitaja wachezaji 125 na Trezquet, akiwemo.

Azizi_Mtambo_15

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here