Home Kimataifa MEZA YA MAKUMBUSHO: Samatta tunakudai

MEZA YA MAKUMBUSHO: Samatta tunakudai

3445
0

Mbwana Samatta wewe nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania. Unacheza Genk na ni kinara wa mabao huko kwa wazungu, wazungu siku hizi wanakuimba lakini hapa kwetu Chama anaimbwa zaidi kwa siku za hivi karibuni kwa kusaidia Simba kwenda robo ACL.

Anaandika @Privaldinho (Instagram)

Samatta bado tunalilia rekodi ya mwaka 1980 ambapo tulishiriki hatua ya makundi AFCON kwa mara ya kwanza na ya mwisho kufikia sasa.

Kitambaa chako kimenikumbusha nahodha pekee aliyewahi kutuwakilisha katika mashindano hayo, naye si Mwingine ni Jella MtagwaMtagwa ndiye aliyehakikisha iwe kwa damu, jasho au moto lazima Stars inapata alama 1 au 3 pale Dag Hammarskjoeld jiji Ndola Zambia. Stars ilifanikiwa kutoka sare ya 1-1 dhidi ya Chipolopolo na kufuzu.

Kama Mtagwa alipigana kufa na kupona kutupeleka Kule Lagos tena akiwa katika ardhi ya wazambia, Samatta utashindwa kweli kuongoza jeshi lako ndani ya uwanja wetu wa taifa?

Samatta umepata mafanikio makubwa sana ndani ya soka mara 100 ya bwana Mtagwa ambaye heshima yake inafifisha mafanikio yako kwenye mioyo ya wapenzi wa taifa stars na heshima ya taifa letu kwako.


Mechi ya kwanza Mtagwa aliwaongoza akina Raisi wa zamani Mh Tenga kuwafumua Chipolopolo pale uhuru kwa goli moja tu.

Mechi ya pili akaenda kulazimisha sare, tukafuzu,.. Samatta ukiwa na akina Msuva mlipata sare kule Uganda, hapa kwetu tunahitaji ushindi tu.

Hapa kwetu Clatous Chama ametawala midomo ya wengi, tunakuomba mwenye mji wako urudi…, Come oooooon Captain Diego

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here