Home Ligi BUNDESLIGA Messi, Zlatan, Sanchez, Ozil, Mata na wachezaji wengine 34 ambao watakuwa huru...

Messi, Zlatan, Sanchez, Ozil, Mata na wachezaji wengine 34 ambao watakuwa huru kuanzia January 1

11815
0

Ijumaa ya tarehe 1, December, Lionel Messi atakuwa yupo huru kujadiliana na timu nyingine yoyote kwa ajili ya kujiunga nayo kwa uhamisho huru, inashangaza lakini ni kweli.

Japokuwa Barcelona wanatoa ishara kwamba Messi ameongeza mkataba, lakini ukweli ni kwamba mkataba wa Messi unamalizika June 2018.

Hivyo kumaanisha kwamba: kutoka January 1 yupo huru kuanza majadiliano na timu nyingine yoyote.

Hata hivyo, sio vyote ving’aavyo ni dhahabu.

Yoyote atakayehitaji huduma za Messi itamlazimu kutoa mkataba mkubwa zaidi kuliko wowote ule aliowahi kupewa Mchezaji yoyote duniani.

Mkataba unaokadiriwa kufikia thamani ya zaidi ya Euro million 30 ambazo anapewa Neymar na Paris Saint Germain.

Ikiwa Messi hatosaini rasmi mkataba mpya na Barcelona na akaonyesha nia ya kuondoka, basi vita ya kuipata saini yake itakuwa kubwa sana.

Kuna siku angalau 38 mpaka kufikia mwishoni mwa mwaka, lakini ikiwa Messi hatosaini mkataba mpya basi kutakuwa na sherehe zaidi ya mwaka mpya.

Hata hivyo sio Messi tu ambaye atakuwa huru.

Kuna wacheza 37 ambao nao mikataba yao inaisha mwishoni mwa msimu na watakuwa huru kuanza kutafuta timu mpya mwishoni mwa mwaka.

Golini unakutana na magolikipa wakongwe Gigi Buffon na Ikea Casillas wakiwa na na mdogo wao Kepa.

Kwenye ulinzi, Chiellini na Miranda wanaungana na Daley Blind kushoto na kulia Juanfran Torres.

Katika kiungo, mjerumaji Leon Goretzka, ambaye anawindwa na Barcelona. Mchezaji mwenyewe ameshaonyesha wazi hana nia ya kubaki Schalke 04.

Ander Herrera, ambaye ana thamani inayofikia 30 million euros, ataungana nae, na Fernandinho atafunga ukurasa hapo katikati.

Kwenye ushambuliaji ndio kuna uimara zaidi.

Wachezaji wakubwa watatu ndio watakaounda safu hiyo.

Mjerumaji Mesut Ozil ataungana na Alexis Sanchez na pembeni yao atakuwepo Lionel Messi.

Hii ndio listi ya wachezaji 37 wakubwa ambao wanamaliza mikataba yao mwaka 2018.

1 Kepa (Athletic)

2 Buffon (Juventus)

3 Casillas (Porto)

4 Reina (Napoli)

5 De Vrij (Lazio)

6 Chiellini (Juventus)

7 Miranda (Inter)

8 Vida (Dinamo Kiev)

9 Daley Blind (United)

10 Ghoulam (Napoli)

11 Shaw (United)

12 Juanfran (Atletico)

13 Joel Ward (Crystal Palace)

14 Glen Johnson (Stoke City)

15 Emre Can (Liverpool)

16 Fernandinho (City)

17 Sung-Yong Ki (Swansea)

18 Motta (PSG)

19 Ander Herrera (United)

20 Leon Goretzka (Schalke 04)

21 Wilshere (Arsenal)

22 Moutinho (Monaco)

23 Cabaye (Crystal Palace)

24 Ribery (Bayern)

25 Ashley Young (United)

26 Mesut Ozil (Arsenal)

27 Juan Mata (United)

28 Ross Barkley (Everton)

29 Mario Balotelli (Niza)

30 Zlatan Ibrahimovic (United)

31 Fernando Torres (Atletico)

32 Alexis Sanchez (Arsenal)

33 Bernard (Shakhtar)

34 Lautaro Acosta (Lanus)

35 Leo Messi (Barcelona)

36 Arjen Robben (Bayern)

37 Aaron Lennon (Everton)

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here