Home Kitaifa “Messi ni kiumbe kingine”-Shaffih Dauda

“Messi ni kiumbe kingine”-Shaffih Dauda

3632
0

Mjadala wa nani mchezaji bora wa muda wote kati ya Legend wa Argentina Diego Maradona na mnyama Lionel Messi umezidi kupamba moto.

Sir Alex Ferguson ameungana na mkongwe wa Scotland na Liverpool Graeme Souness kusema Messi ni bora zaidi ya Diego Maradona kwa sababu Messi amedumu kwenye kiwango cha juu kwa muda mrefu lakini Maradona alikuwa bora kwa miaka michache.

Edo Kumwembe amesema amewashuhuia wote Maradona na Messi, kwake Messi anabaki kuwa mchezaji bora wa muda wote mbele ya Maradona.
.
Kwa upande wangu mimi, Messi ni bora zaidi ya Maradona. Messi anashikilia rekodi ya kupiga pasi za mwisho na ufungaji wa muda wote kwenye timu ya taifa ya Argentina.

Kuna watu wanasema Messi akiwa Barcelona ndio anaonekana bora kwa sababu anacheza mbele ya watu bora ndio maana akiwa na timu ya taifa Argentina hakuna anachofanya.
.
Wote ni mashahidi miezi kadhaa iliyopita tulikuwa tunaangalia kombe la dunia, Argentina ilikuwa ipo hovyo lakini Messi kama nahodha alionekana anavyopambana uwanjani.

Watu wengine wa asema Messi amecheza ligi moja aende sehemu nyingine tuone…maisha hayapo hivyo, mtu anapimwa kwa kitu alichonacho. Iniesta, Xavi, Lampard, Scholes na wengine hawakuhitaji kucheza ligi nyingi tofauti ili kuuthibitishia ulimwengu ubora wao.

Wapo wanaosema Messi hana kombe la dunia lakini hapa tunazungumzia ubora wa mtu mmoja mmoja, kushinda kombe la dunia ni ishu ya timu na sio uwezo wa mtu mmoja.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here