Home Kimataifa Mchezo Wa NBA Afrika Kupigwa Tena. Makampuni Yajitokeza

Mchezo Wa NBA Afrika Kupigwa Tena. Makampuni Yajitokeza

4134
0

Chama cha mpira wa kikapu chini Marekani (NBA) and pamoja na chama cha wachezaji wa mpira wa kikapu nchini Marekani (NBPA) wametanganza kuwa makampuni ya Kwesé Sports, Ford Motor Company kutoka Afrika Kusini, Castle Lite, General Electric, Solektra International, Marriott International pamoja na 947 kuwa watakuwa sehemu ya NBA Africa Game 2017.

Hii itakuwa mara ya kwanza kwa mchezo wa NBA unaofanyika Afrika maarufu kama NBA Africa game kuwa na idadi hii kubwa ya wenza washiriki tangu uanze kufanyika.

Mchezo huu ambao utakuwa wa pili kufanyika Afrika utafanyika siku ya Jumamosi tarehe 5, aktika uwanja wa Ticketpro Dome huko Johannesburg, South Africa.

NBA Africa Game 2017, ambao utafanyika ikiwa ni baada ya uzindiuzi wa awamu ya 15 ya mpira wa kikapu bila mipaka which [Basketball without Borders (BWB)] kwa Africa, utafanyika tena ukiwahusisha wachezaji watakaogawanywa kwenye timu mbili ambazo Team Africa vs Team World na utachezwa ikiwa ni katika kuwaunga mkono UNICEF, Nelson Mandela Foundation na shirika la SOS Children’s Villages South Africa (SOSCVSA).

Team Africa, ambayo itakuwa na wachezaji Bismack Biyombo (Orlando Magic; Democratic Republic of the Congo) pamoja na Emmanuel Mudiay (Denver Nuggets; Democratic Republic of the Congo), itajumuisha pia wachezaji kutoka Afrika na wale wenye asili ya Afrika. Team World, ambayo itakuwa na CJ McCollum (Portland Trail Blazers; U.S.), itakuwa na ongezeko la wachezaji kutoka nchi nyingine duniani.

Taarifa zaidi juu ya vikosi kamili, makocha na wachezaji wengine wa zamani wa NBA itatangazwa siku nyingine zijazo.

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here