Home Kitaifa Mbeya City yafafanua mchezaji wake kufanya majaribio Misri

Mbeya City yafafanua mchezaji wake kufanya majaribio Misri

3881
0

Uongozi wa Mbeya City umetoa ufafanuzi kuhusu mchezaji Eliud Ambokile ambaye kupitia mitandao ya kijamii na baadhi ya vyombo vya habari vimeripoti anakwenda Misri kwa ajili ya majaribio.

Mtendaji Mkuu wa klabu ya Mbeya City Emmanuel Kimbe ameeleza juu ya taarifa zilizoenea kwamba Eliud anaenda kufanya majaribio kwenye klabu ya El Gouna FC.

“Hilo jambo bado lipo katika hatua za awali sana lakini kuna watu wameamua kulikuza tu si dhani kama lipo hivyo.”

“Mipango ya kwenda kufanya majaribio ipo, klabu inafanya hivyo na sio mara ya kwanza. Bahati mbaya siku za nyuma klabu ilitaka kuwapeleka nje wachezaji wakafanye majaribio lakini waliondoka kabla muda haujafika.”

“Plan hiyo ipo kwa muda mrefu na imemkuta Eliud akiwa bado ndani ya klabu. Mpango wa kumpeleka Eliud kwenye majaribio upo lakini bado haujawa tayari ndio maana klabu haijatangaza kuhusiana na hilo. Mipango itakapokuwa imekamilika klabu itatoa taarifa rasmi.”

Kimbe amesema Eliud hana wakala wala meneja anaemsimamia zaidi ya klabu ya Mbeya City FC na kuwataka wale wote wanaojitangaza mameneja wa mchezaji huyo kuacha kufanya hivyo.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here