Home Kimataifa Maximo vs Amunike

Maximo vs Amunike

5531
0

Wahenga walisema yakale hayanuki. Kwa haya yanayotukumba watanzania kuna haja ya kutafuta mchawi ni nani. Kwanini tuanze kuulizana habari za miaka iliyo pita ili hari wahenga walishasema yaliyo pita si ndwele, tugange yajayo!!

Mnapo mwaka 2010. Taifa starz ilikua chini ya mwalimu Marcio Maximo ambaye alikua na tumaini kubwa la kuibua soka la nchi yetu. Alitangaza moja ya kikosi ambacho kilicheza dhidi ya Uganda the cranes. Ambacho kilikua asilimia mia cha wachezaji wanaocheza ligi ya Tanzania.

Aliwataja wachezaji hao na timu wanazotoka katika mabano ni Makipa, Shabaan Shaaban ‘Kado’ (Mtibwa Sugar) na Jackson Chove (JKT Ruvu), Mabeki ni Shadrack Nsajigwa na Nadir Haroub (Yanga), Salum Kanoni, Juma Jabu, Kelvin Yondani na David Naftari (Simba), Stephano Mwasika (Moro United) na Aggrey Morris (Azam FC).
Wengine ni Abdulhalim Humuod na Shaaban Nditi (Mtibwa), Erasto Nyoni (Azam), Juma Nyoso (Simba), Abdi Kassim, Kigi Makasi na Nurdin Bakari (Yanga), Mbwana Samatta (African Lyon) na Ibrahim Mwaipopo (Azam) na washmabuliaji ni Mussa Hassan ‘Mgosi’ (Simba), Mrisho Ngassa na Jerson Tegete (Yanga) John Bocco (Azam).
Mkongwe Saalum Swedi aliomba kuustaafu ili kupisha vijana waendeleze gurudumu la taifa. Kuleta ladha tamu kwa mashabiki.
Aidha Mwaka 2009, Starz ya Marcio Maximo iliichapa Taifa la New zealand kwa mabao 2-1. Na kuushangaza ulimwengu.

Hiki ndicho kikosi kilichocheza dhidi ya New Zealand

TUNAKWAMA WAPI? na mwalimu Emmanuel Amunike.

September 2018, mwalimu Amunike aliita kikosi cha wachezaji 30, ambao walifufua matumaini ya watanzania . aliwajumuisha
Makipa Aishi Manula, Beno Kakolanya, Mohammed Abdulahim, Mabeki Hassan kessy, Shomari Kapombe, Salum Kimenya, Gabriiel Michael, Paul Ngalema, Ally Sonso, Aggrey Morris, David Mwantika, Abdallah Kheri, Kelvin Yondan, Andrew Vicent, Abdi Banda Viungo Himid Mao, Simon Msuva, Frank Domayo, Jonas Mkude, Feisal Salum, Salum Kihimbwa ,Farid Mussa Washambuliaji Mbwana Samatta, Thomas Ulimwengu, John Bocco, Yahya Zaid, Kelvin Sabato, Rashid Mandawa, Shaaban Chilunda.
Swali la msingi, tunakwama wapi watanzania?.

Tuna wachezaji wakubwa hapa Tanzania na wanao cheza ligi kubwa za Afrika na nje ya Afrika. Swala la kuwekeza kwa vijana lilisha shindikana. Tunasubiria timu ioneshe mwanga ndo harambee na michango inaanza kupitishwa, tunachokua tunakifanya ni sawa na kurisha mbuzi nyasi mbuzi siku ya mnada. Kwa nini tusiwekeze mapema na kuweka malengo kwa kila mwaka?. Kwa usawa huu nasema yakale huwa hayanuki lakini yakinyeshewa na mvua huwa mapya.kwa nini tujiite kichwa cha mwendawezamu wakati ueledi na werevu tunao?, kwa nini tuwe daraja la mataifa mengine kujizoelea pointi na kwenda kushiriki michuano ambayo sisi pia tungeweza kushiriki Kipigo kilicho patikana dhidi ya mechi ya Lesotho ni maumivu makali kwa watanzania wote wenye uzalendo na nchi yao.

Mamlaka husika, tusijisahau kilicho tukumba katika hatua ya makundi. Na sasa tupo katika nafasi ngumu inayoshikiliwa na kipande cha uzi. Mimi naamini siku moja tutakua moja kati yao, imetosha sasa miaka 38 ni kipindi kirefu cha aibu kwa nchi inayopenda soccer kama Tanzania. Sio kwamba lazima tushiriki AFCON 2021, bali tuanze hatua ya kujiandaa kwa ajiili ya michuano inayofuata baada ya hapo. Ama sivyo. Tuendelee kunywa supu nyama zipo chini.
Mwandishi ISACK MSINJILI

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here