Home Kitaifa Maxime apokea kipigo kwa mikono miwili

Maxime apokea kipigo kwa mikono miwili

2933
0

Kocha wa Kagera Sugar Mecky Maxime amesema wamepoteza mchezo (3-2) dhidi ya African Lyon kwa sababu walifanya makosa mengi.

“Mechi ilikuwa ngumu lakini tumepoteza kutokana na kufanya makosa mengi na wenzetu wakayatumia na siku zote ukifanya makosa unaadhibiwa”-Mecky Maxime.

“Bado tunapambana kwenye ligi, unaposhinda unasogea juu unapofungwa unashuka. Raundi ya pili ndio imeanza na sasa ndio mechi ya pili.”

“Nawamini wachezaji wangu tunarudi Bukoba kujipanga kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya Biashara Jumamosi ijayo.”

Kagera itasafiri kwa siku mbili njiani kuelekea Bukoba ulipo uwanja wake wa nyumbani (Kaitaba), inatarajia kufika siku ya Ijumaa, Jumamosi watapumzika Jumapili jioni watacheza.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here