Home Kimataifa Mauricio Pochettino muosha dhahabu za kiingereza

Mauricio Pochettino muosha dhahabu za kiingereza

4438
0

POCHETTINO amekuwa Kocha anaesifika ulimwenguni kwote kwa namna yake ya kipekee aliyokuja kuongeza wigo wa ligi ya England baada ya kuita Big four sasa wanaita TOP six. Tangu awasili katika Ligi ya England amekuwa kocha aliefanikiwa zaidi kwa kipindi hiki cha Miaka 6. Alicheza vilabu vya Espanyol PSG na Bodeaux.

Ameitumikia timu ya taifa Argentina katika Kombe la Copa America mwaka 1999 pamoja na Kombe la Dunia mwaka 2002.

Alianza majukumu yake ya ukocha akiwa katika Klabu yake ya Espanyol mwaka 2009/Jan. Katika Kipindi chake cha ukocha mechi yake ya kwanza ilikua dhidi ya FC Barcelona iliyokua ikiongozwa na kocha Pep Guardiola na katika mechi hiyo ilimalizika kwa Espanyol kuenda sare ya bila kufungana.

Aliikuta katika nafasi za chini kwenye msimamo wa ligi. Lakini kwa mpaka wanaelekea mwisho wa msimu timu ilifika katikati ya msimamo jedwali la msimamo wa ligi.

Aliiongoza Espanyol kwa kipindi cha miaka minne(4) na kujiunga na Southamptom nchini England 2013. Alikuwa kocha mdogo kuliko wote Ligi kuu nchini England (35). Changamoto kubwa kwake ilikuwa lugha. Aliomba msaada wa wakalimani kumsaidia.

Msimu wa kwanza alitoa dozi kali kwa timu kubwa kama Man city 3-1, Chelsea 2-1, Liverpool 3-1. Alimaliza msimu wa kwanza akiwa mafasi ya 8 na kuweka rekodi ya kumaliza nafasi ya juu kwa klabu hiyo tokea 2002-2003.

Mwaka 2014 akajiunga Tottenham Hotspurs na mkataba wa miaka 5. Msimu wake wa kwanza alianza ligi akiwa na wachezaji wadogo waliokulia katika kademi ya Timu hiyo. Wachezaji hao walikua ni Harry kane, Roberto Soldado, Delle Alli, Eric Dier.

Msimu wa kwanza akamaliza nafasi ya 5. Ilikua ni gumzo kubwa kupitia timu hii ambayo ilimkaribisha Kane katika ulimwengu wa kupachika nyavu nchini England.

Ana sifika sana kwa soka la kushambulia kwa kasi huku Mabeki wake wakihusika katika Kupandisha mashambulizi mfumo wa 4-2-3-1. Alifanikiwa kuingia TOP 4 kitu na kuwashawishi mabosi wake. Aliendelea na mfumo wakupandisha vijana timu ya wakubwa na kufanya nao kazi.

Mwaka jana katika kombe la dunia England ilishika nafasi ya 4 huku ikitawaliwa na wachezaji wanaocheza ligi ya ndani. Kikosi cha kwanza kilitawaliwa na Dele Ali, Erick Dier, kieran Trippier, Danny Rose na Harry Kane.

Wakati tunapongeza England kumbukeni kuna Pochettino nyuma ya hili taifa katika soka.

Ameweza kuosha dhahabu iliokua katika tope. Uthubutu wake umeendelea kushangaza ambapo mpaka sasa hajapewa pesa ya kusajili kwa misimu miwili. Lakini hiyo haijawa kizuizi kuendelea kung’ang’ana na top four mpaka sasa watu wameongeza wigo wanaita Top six ili timu zao zitajwe( jokes) tehtehteh.

Ana miaka 46 nina muona mbali katika hii tasnia ya wakufunzi.

Mkimuandika Kane katika uwanja mpya wa White Hart lane Msimsahau na Pochettino.

Cc.@sativa_clan.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here