Home Kimataifa Matokeo ya michezo mikubwa ya kimataifa iliyopigwa leo

Matokeo ya michezo mikubwa ya kimataifa iliyopigwa leo

12786
0

Wales 4-Ireland 1. Gareth Bale alifunga moja ya bao la Wales na kumfanya kuwa nyota wa kwanza kufikisha mabao 30 katika timu hiyo.

Mabao mengine ya Wales katika mchezo huu yaliwekwa kimiani na Tom Lawrance, Aron Ramsey na ConnorRoberts huku lile la Ireland likiwekwa kimiani na Shaun Williams.

Uholanzi 2-Peru 1. Walianza kutangulia Peru katika dakika ya 17 tu ya mchezo kwa bao ambalo liliwekwa kimiani na mshambuliaji Pedro Aquinho.

Lakini Uholanzi walirudi katika mchezo huo kwa bao la kusawazisha la Memphis Depay dakika ya 60 kabla ya dakika ya 82 kufunga lile la ushindi.

Mchezo wa leo wa Uholanzi ulikuwa mchezo wa mwisho kwa kiungo Wesley Sneijder kuitumikia timu hiyo ambayo ameshaichezea michezo 134.

Katika michezo hiyo 134 Sneijder alifanikiwa kushinda kufunga mabao 31 akitoa assists 31 huku akiwa katika kikosi kilichofika fainali ya kombe la dunia 2010.

Portugal 1-Croatia 1. Portugal wakiwa bila Cristiano Ronaldo iliwabidi kumtumia Pepe kusawazisha goli dakika ya 32 baada ya Ivan Perisic kutangulia kuwafungia Croatia dakika ya 18.

Katika michezo mingine mikubwa ambayo imepigwa hii leo, mabingwa wa dunia Ufaransa walitoshana nguvu na timj ya taifa ya Ujerumani kwa kwenda sare ya bila kufungana.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here