Home Kimataifa Matic anawaumbua waliombeza

Matic anawaumbua waliombeza

5042
0

Nemanja Matic raia wa Serbia mwenye umri wa miaka 30 anaekipiga katika klabu ya Manchester united kwa sasa. Alinunuliwa kutokea Chelsea ambayo ilikua imetoka kutwaa ubingwa wa Epl chini ya Konte. Alionekana kushawishika sana kujiunga na Manchester united kutokana na uwepo wa kocha wake wa zamani akiwa chelsea Jose Mourinho.

Kitu ambacho hakifahamiki kutoka kwa Matic nikua Matic alikua ni mchezaji wa chelsea tangu mwaka 2009 na amekua akitolewa kwa mkopo mpka alipokuja Kocha Josse Mourinho mwaka 2014 alipo mrudisha Rasmi kutokea klabu ya Benfica


Huu ulikua msimu wa mwaka 2014/2015 aliweza kutwa ndoo ya EPL akiwa na kocha wake Josse mourinho mwaka unaofuata 2015/2016 Josse alitimuliwa klabuni hapo na kuiacha Chelsea ikimaliza msimu ya 10. Msimu wa 2016/2017 huu ulikua msimu wa Kocha Antonie Konte alieweza kutwaa kombe la Epl na kumfanya Matic kubeba Ndoo za ligii kuu England mara mbili. Lakini msimu huo ndo mourinho alikua ashaitumikia united msimu mmoja na kufanikiwa kubeba Europa na Efl.

Hapo ndipo msimu 2017/ 2018 wakaungana na kocha wake aliemleta katika mafanikio yote haya. Lakini hakumfaidii sana baada ya mwishoni mwa mwaka 2018 mwezi Disemba kutimuliwa kocha josse Mourinho katika klabu yake ya united.


Wakati Manchester united inapambana sana kutafuta matokeo kipimdi cha mourinho ilifikia hatua mashabiki wakaanza kuona kama anamkumbatia Matic kwa kiwango chake kuonekan a ni dhaifu. Na hii ilikua msimu wake wapilii ambao mourinho alitimuliwaa. MATIC alikua hachezi kwa faida uwanjani alionekana kama mtalii .

Sasa tangu amekuja Ole Gunnar kunatofauti kubwa sana pale katikatii ambapo unakuta muunganiko wa Herrera na Matic. Matic amekua nauwezo wa kuzuia vizuri lakini amekua na uwezo kuanzisha mashambulizi vile ipasavyo. Wamejenga undungu kati yake na herrera na kufanya Pogba aonekane.


Ikumbukwe Matic wa msimu wa kwanza alipojiunga na manchester alikua ndoo muhimili mkuu wa timu lakini msimu huu wakatii unaanza alianza ovyo nazani ni mwalimu mou na mbinu zake. Lakini kwa huyu Matic wa mechi 8 kwakweli tutatubu sanaa.

@sativa_clan

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here