Home Kitaifa Mashindano ya Copa Coca-Cola UMISSETA yazinduliwa rasmi Manyara

Mashindano ya Copa Coca-Cola UMISSETA yazinduliwa rasmi Manyara

4933
0
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Mwita Waitara akisalimiana na washiriki wa mashindano ya Copa Coca-Cola kwa mwaka 2019 wakati wa hafla ya uzinduzi wa mashindano iliyofanyika mkoani Manyara hivi karibuni.

Mashindano ya mwaka 2019 ya Copa Coca-Cola UMISSETA yamezinduliwa rasmi mkoani Manyara leo ikiendeleza juhudi za Kampuni ya Coca-Cola kuunga mkono michezo mashuleni hapa nchini.

Uzinduzi huo umefanyikia katika Uwanja wa Kwaraa wikiendi hii, ambapo mgeni rasmi alikuwa Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI), Mhe. Mwita Waitara.

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Mwita Waitara akisubiria kuvalishwa kitambaa cha Scarf mara baada ya kuwasili mkoani Manyara kwa ajili ya kuzindua mashindano ya mwaka 2019 ya Copa Coca-Cola UMISSETA.

Tukio hilo pia lilihudhuriwa na maofisa mbalimbali wa Serikali, maofisa michezo, walimu na wanafunzi kutoka shule mbalimbali za sekondari mkoani Manyara.

Akizundua michezo hiyo mkoani Manyara, Waitara aliishukuru Coca-Cola kwa kuwezesha michezo ya Copa Coca-Cola UMISSETA kuzinduliwa rasmi mkoani humo kwa mara ya kwanza huku akiwahimiza vijana wa Manyara kuthibitisha vipaji vyao dhidi ya mikoa mingine kupitia mashindano hayo.

‚ÄúNingependa kuwahimiza vijana wa mkoani hapa kuifanya hii michezo kuwa sehemu ya kujifunza zaidi na njia ya kuongeza ushiriki katika shughuli za nje ya masomo. Tofauti na siku za nyuma, Michezo siku hizi ni biashara yenye thamani kubwa, na kila mmoja wenu hapa anaweza kuwa shahidi ya hili,” alisema.

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Mwita Waitara akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa mashindano ya Copa Coca-Cola kwa mwaka 2019 iliyofanyika mkoani Manyara hivi karibuni.

Alibainisha kuwa, kumbukumbu zinaonyesha kwamba kuna idadi kubwa ya vijana mkoani Manyara ambao vipaji vyao viligunduliwa kupitia michezo ya Copa Coca-Cola UMISSETA na sasa wanashiriki katika ligi za juu tofauti tofuati.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Bonite Bottlers mkoani Manyara, Samwel Bitalian alisema, kupitia michezo, Coca-Cola imedhamiria kuwafika wanafunzi wengi nchini kadri iwezekanavyo ili kuwapa fursa ya kushiriki katika michezo hiyo na kuvumbua vipaji.

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Mwita Waitara akifurahia jambo na Mwakilishi wa Kampuni ya Coca-Cola, Pamela Lugenge wakati wa hafla ya uzinduzi wa mashindano ya Copa Coca-Cola UMISSETA kwa mwaka 2019 yaliyofanyika mkoani Manyara hivi karibuni.

Kama sehemu ya udhamini wa mashindano hayo, Kampuni ya Coca-Cola itasambaza vifaa vya michezo zaidi ya 2000 katika shule za sekondari nchini.

Uzinduzi wa mashindano ya Copa Coca-Cola UMISSETA, katika ngazi ya mkoa katika mkoa wa Manyara ni wa tano tangu kuanzishwa kwa michezo hiyo mkoani Dodoma kasha Tanga, Zanzibar na Mtwara. Katika ngazi ya Kitaifa michezo hiyo itafanyikia Uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara mwaka huu.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here