Home Ligi EPL Mapacha waliowahi kusakata kabumbu EPL

Mapacha waliowahi kusakata kabumbu EPL

6580
0

Josh na Jacob Murphy wanatarajia kukutana tena wakati Cardiff watakapokutana na Newcastle, ni mechi ambayo itakutanisha wana ndugu hawa ambao ni mapacha. Jacob na Josh Murphy, walicheza wote pamoja Norwich City kabla Jacob hajajiunga Newcastle mwaka 2017 na Josh kujiunga Cardiff mwaka huu.

Will na Michael Keane, watakutana pale Hull watakapoumana na Burnley. Mapacha hawa wa Keane itakuwa kwa mara yao ya pili kukutana ikiwa ni rekodi ndani ya EpL kwa mapacha kukutana mara mbili wakiwa na timu tofauti. Will alikuwa na Hull kwemye mchezo ulioenda sare ya 1-1 dhidi ya Michael aliyekuwa Burnley mnamo Septemba 2016.

Martin na Marcus Olsson, wanandugu hawa kutoka sweden walicheza michezo 10 wakiwa pamoja katika klabu ya Blackburn 2011/12, kabla ya Martin kumtikia Norwich na baadae Swansea.

Rafael na Fabio Da Silva, mapacha hawa walichezea klabu ya Man Utd. Wote hawa ni wazaliwa kutoka Brazil. Walicheza pamoja msimu wa 2010/11 Rafael alicheza kwa muda mrefu midogo kuliko fabio. Walibahatika kucheza ndani ya Manchester United kwa pamoja mechi tatu tu.

Adam na James Chambers, wote hawa walicheza pamoja West Brom. Mapacha hawa wa Chambers walikiwa mapacha wa pili kuwahi kucheza kwenye timu mbili ndani Premier League, paale walipoifunga Arsenal mabao 2-1 msimu wa 2002/03.

Ray na Rod Wallace, hawa ni mapacha wa kwanza kabisa kupata nafasi ya kucheza ligi kuu England. Wote hawa walichezea Leeds. Rod alicheza mechi 7 ambazo Ray pia alianza akiwa na Leeds United. Rod alifunga mabao 45 kwenhe mechi 197.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here