Home Ligi EPL Man City yaweka rekodi ya pato kubwa kwa mara ya kwanza katika...

Man City yaweka rekodi ya pato kubwa kwa mara ya kwanza katika historia yao.

12705
0

Mabingwa wa ligi kuu Uingereza Manchester City wamewasilisha mapato yao ya msimu uliopita ambapo yanafikia £500.5 millioni sawa na dola ($652 millioni) kwa msimu wa 2017/18. Klabu hiyo pia imefanikiwa kupunguza idadi kubwa ya mishahara kwa wachezaji wake.


English champions wanavyojiita wenyewe, Manchester City chini ya utawala Pep Guardiola waliweka rekodi ya kufikisha alama 100 na kutwaa ubingwa huo.

Vipi kuhusu faida waliyopata?

City wamepata faida ya £10.4milioni, kwa mwaka wa 4 mfululizo lakini kubwa zaidi mishahara ya wachezaji imepungua hadi kufikia asilimia 52. Mwanzono klabu ya Man city ilikuwa inalipa wachezaji miashara minono sana lakini ujio wa Pep umepunguza mishahara hiyo.

Mabosi wanasemaje?

“Bado hatujafikia malengo yetu, tuna mengi ya kutimiza,” Alisema mwenyekiti wa klabu hiyo Shekh Khaldoon Al Mubarak.

Mubarak hivi majuzi alikuwa akisheherekea miaka 10 tokea familia hiyo ya Abu Dhabi kichukua mikoba ya kuiendesha klabu hiyo.

.”Bila shaka tuna mitazamo ya mbele, tunafaham zipo changamoto nyingi mbele yetu, na tunajitoa kwa moyo wetu kama miaka 10 iliyopita”


Raheem Sterling anatamani mshahara wake wa sasa £100,000 kuongezwa hadi kufikia angalau £175,000 kwa wiki kama Manchester City watataka kumpa mkataba mpya.

Sterling anatarajia kupokea £275,000 ikiwa hiyo ni pamoja na bonasi zote za matangazo na haki za picha.


Hapo awali Man City walikuwa wanapata kiasi gani?

Kabla ya Sheikh Mansour kuchukua Man city, ilipata faida ya £87 millioni kwa msimu wa 2007/08. Klabu hiyo hapo awali haikuwa na majina makubwa sana na uwekezaji wake ulikuwa wa kawaoda tofauti na sasa.

Penye mafanikio hapakosi changamoto, Je Man City wamepata hasara yeyote kwa kipindi cha miaka 10?

Ndio. Baada ya uwekezaji huo mkubwa Man City walipata hasara ya £584 millioni kwa miaka 6 iliyofuata kutokana na matumizi mkubwa waliofanya, ikiwemo usajili wa majina makubwa kama vile akina Robinho n.k.

Matumizi mengine mbali na usajili?

Mansour alifanya mabadiliko makubwa sana ndani ya klabu hiyo. Hapo awali walitumia zaidi ya £200 millioni kuboresha uwanja wa mazoezi wa Etihad Campus training ground.

Wamerudiaha vipi gharama zao?

Kama tunavyojua klabu ikiwa na majina makubwa baraka zinaanza kuja zenyewe. Man city ilianza kupata ofa nyingi za Tv, na uhasama wao mkubwa wa nje na ndani ya uwanja dhidi yao mahasimu wao Manchester United kuliwapatia jina kubwa na mvuto wa kibiashara uliongezeka kwa wawekezaji na mechi zao kuanza kufuatiliwa sana.

Kwingineko?

Mbali na ushindani wao ndani ya Uingereza pia ushiriki wao wa mara kwa mara ya michuano ya ulaya kwa miaka ya hivi karibuni kuliwaweka kwenye kundi la vigogo wa bara la ulaya kama Barcelona, Real Madrid na Bayern Munich kuliwaongezwa pato kubwa. Unapokutana na timu kunwa kama hizo mechi zakp zitafuatiliwa na mashabiki wengi duniani wataanza kufuatilia timu yako.


Kwa ufupi

Kocha wa Man City Pep Guardiola amesema kuwa kiungo wake Kevin De Bruyne thamani yake ni Euro 222M


Michezo ya wikiendi hii

SEP 9–SEP 15

 

SEP 16–SEP 18

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here