Home Kimataifa Makosa ya Wawa akiyafanya Mlipili tungesema sana.

Makosa ya Wawa akiyafanya Mlipili tungesema sana.

3856
0

Yaweza kua jina la Mchezaji wa kimataifa ndio linalowabeba baadhi ya wachezaji wanaocheza hapa nchini kwetu wakitokea mataifa mengine lakini kiuwezo wanaweza kulingana au kuzidiwa na wachezaji wazawa wa hapa Tanzania, Najiuliza tu kwa faida ya wachezaji wetu wazawa hivi tukitengeneza mazingira rafiki ya kiushindani hatuwezi kua kiwanda cha kuzalisha akina Samata Watano sio kuleta akina Wawa wanne?

Ok basi turudi kwenye maada tajwa juu, Jana wawakilishi wa nchi yetu kimataifa Simba sports club walikua uwanjani kucheza ugenini dhidi ya waarabu wa Aljeria Js Saoura na matokeo ya Simba kupoteza kwa mabao mawili kwa sufuri, mchezo ambao Simba ilicheza pasipo na wachezaji wake muhimu Emanuel Okwi, Juuko Murshed, Na walio na majeraha akina Kapombe.

Tatizo halipo kwenye kukosa wachezaji tatizo ni aina ya kufanya marekebisho ya kimfumo na kiuchezaji Kwani Kuna aina ya makosa ambayo yanajirudia kila siku ambayo yanafanywa na beki wa kati Paschal Wawa, makosa ambayo yananifanya kumkumbuka beki kisiki Yusuph Mlipili dhidi ya Al Masry ambapo alicheza vizuri na tokea pale simuoni tena ndani ya kikosi cha wana Msimbazi simba. Matatizo yalianzia upande wa kulia ambako anacheza Zana Coulibaly na kusababisha kuwepo na mashimo mengi eneo la ulinzi lililokua linaongozwa na Wawa pamoja na Bukaba, Pamoja na kusababisha penati na pasipo hekima na mwamuzi labda tungesemea penati zaidi ya moja lakini binafsi Paul Bukaba alilitendea Haki eneo lake la ulinzi tofauti na Wawa ambae amekua akifichwa na kivuli cha majeruhi kwa baadhi ya wachezaji kwamba ana uwiano mzuri na walio namajeraha kitu ambacho sicho sahihi Bali Wawa amekua na makosa mengi hasa pale simba wanapokua wanashambuliwa kwa nguvu na wapinzani

Katika mechi tatu za ugenini ambazo Simba amepoteza kwa mabao 12 pasipo kupata chochote Wawa amekua akionekana kukaba kwa macho zaidi pamoja na kukosa uwezo wa kukimbizana na kupunguza pressure kwa wapinzani wao, kitu ambacho kama kingefanywa na mchezaji wa ndani yaweza kua Wanasimba wangeongea na zaidi ata nafasi yake kwenye kikosi huenda ingepotea, ni jukumu la kocha kuangalia jinsi ya kutengeneza uwiano mzuri kwa mabeki Kwani kocha anaamini uwezo wa Wawa na Bukaba na kukosa nafasi kwa beki king’ang’anizi Yusuph Mlipili, Aussems kumbuka Una mechi ngumu dhidi ya As vita ambao wanaamini robo fainali wanafika kwa kupitia tiketi yenu

by Raphael Lucas
0764764449/0710690782

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here