Home Kitaifa Makambo OUT JKT Tanzania vs Yanga

Makambo OUT JKT Tanzania vs Yanga

3829
0

Kuelekea mchezo wa ligi kuu Tanzania bara JKT Tanzania vs Yanga kwenye uwanja wa Mkwakwani Tanga, Yanga itamkosa mshambuliaji wake Heritier Makambo ambaye atakuwa akitumikia kadi tatu za njano.

Mratibu wa timu hiyo Hafidhi Saleh amethibitisha kukosekana kwa nyota wao mpasia nyavu.

“Tutamkosa Heritier Makambo, ana kadi tatu za njano kwa hiyo hatokuwa sehemu ya mchezo dhidi ya JKT Tanzania.”

JKT TANZANIA vs YANGA

“Hakuna timu ndogo kwa sababu kila timu inapigania ipate pointi tatu muhimu. Sisi tulifanya makosa dhidi ya Coastal Union na Singida United, mwalimu amerekebisha makosa ambayo yalifanyika kwa hiyo wachezaji wanajua wamerekebisha nini na tunaweza kupata ushindi.”

RATIBA IMEBANA

“Ratiba imebana sana kwa sababu mchezo wa mpira wachezaji wanatakiwa kucheza na kupumzika. Jana (Alhamisi) tumeanza safari saa 12 asubuhi kutoka Singida tumefika Tanga saa 4 usiku utaona kwamba wachezaji wamecheza mechi hawajapumzika wameingia kwenye safari ya saa 12 hadi 14 sio nzuri.”

“TFF na Bodi ya Ligi waliangalie wachezaji wacheze halafu wapumzike.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here