Home Kitaifa Magufuli alivyoongoza maelfu kumuaga Ruge Dar

Magufuli alivyoongoza maelfu kumuaga Ruge Dar

2713
0

Alizaliwa Marekani (01/05/1970). Alisoma darasa la kwanza hadi la sita huko Arusha School, akaja kumaliza hapa DSM katika shule ya msingi Mlimani.

Baadae alienda Forodhani Secondary na kisha kumaliza Pugu Secondary. Kisha alienda Marekani kusoma, na akamaliza Shahada ya Marketing huko San Jose University.

Hayo ni maisha yake ya Shule, alifaulu vizuri lakini bado alitamani muziki. Alirudi nyumbani kuupambania Muziki.

Alikuwa na vipaji vingine ikiwemo kucheza mpira. Akiwa sekondari alikuwa anapiga mpira mwingi hadi alichaguliwa timu ya mkoa.
Na wakati huo alikuwa pia ameanza kujaribu kuandika vitabu.

Lakini mapenzi yake kwenye muziki yalizima talanta nyingine zote.

#RugeMutahaba ameacha watoto 5. Mkubwa ni huyu Mwachi ambaye amesoma wasifu wa baba yake hapa (Juu pichani).
Wengine wanne wapo hapo (Chini pichani).

Nyuso za majonzi zikiwa ndiyo zimetawala kwa watoto wa mpendwa wetu Ruge Mutahaba.

Wasanii wa THT (Watoto wa Ruge) wakiwa tayari hapa #KarimjeeHall ili kuhakikisha wanatoa salamu zao za mwisho kwa Baba yao mpendwa Ruge Mutahaba.

Baadhi ya wasanii wakiwa na sura zilizosawajika majonzi hapa #KarimjeeHall ili kuweza kushiriki kumuaga mpendwa wetu Ruge Mutahaba (Monalisa, JayMelody na Bushoke).

 

Ukumbi wa Karimjee ni hadhi ya aina yake: hapa ndipo Baba wa Taifa, Hayati Julius Nyerere aliapishwa kuwa Rais wa Kwanza wa Tanzania na hapa ndipo lilipokuwa Bunge la Tanzania.

Na hapa ndipo alipoagwa.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk, John Pombe Magufuli akisalimiana na wazazi wa Ruge Mutahaba hapa kwenye viwanja vya #KarimjeeHall

Familia ya #RugeMutahaba wamesema wanatambua Ruge aliwahi kuwakosea watu kwa kuwa yeye ni binadamu hajakamalika. Mtoto mkubwa wa Ruge amesema “Familia inaomba msamaha kwa niaba yake.” Lakini pia wapo waliomkosea Ruge na pengine wapo wanaoendelea kumkosea. Familia imesema “TUMEWASAMEHE WOTE….TUENDELEE MBELE.”

“Baba alikuwa kinara” Mwachi mtoto mkubwa wa mpendwa wetu Ruge Mutahaba,
Kinara ni neno lenye tafsiri kubwa sana na wengi ambao wanabubujikwa na machozi na nyuso zenye makunyazi ya uchungu wao kwao Ruge ni kinara na kaweza kugusa maisha ya watu wengi.

“Siku nikifa Jo msilie…haya yalikuwa maneno siku nilipoenda India nilienda kwa surprise. Alinikumbatia, it was a warm hug ever, and it was the last hug i had from him” ni Joseph Kusaga akisema kwamba rafiki yake alimkumbati kwa nguvu wakiwa India na hiyo ndiyo mara ya mwisho yeye kumkumbatia.

“Ruge alitengeneza kina Ruge wengine wengi wapo Clouds….na mimi binafsi kupitia Foundation nitahakikisha tunaendeleza yale aliyokuwa akifanya #RugeMutahaba.”

“Ndugu zangu, Wasanii wa nchi na Muziki ulikuwa unaitwa uhuni. Lakini Ruge Mutahaba alifanikiwa kuufanya utumike katika kazi za Kijamii. Rais Mstaafu Kikwete tena anakumbuka kuhusu project ya (Zinduka/ Malaria No More) yule ndiye Ruge tunayesherehekea maisha yake hapa. Kwa wasiojua, kutokana na mafanikio ya Mradi ule hapa Tanzania, Nchi za nyingine za Afrika mfano Ivory Coast, zilimchukua Ruge na akawasaidia katika miradi ya namna hiyo. Tukisema Afrika inalia tunamaanisha.”

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli akitoa salamu zake za mwisho kwa mpendwa wetu Ruge Mutahaba.
Ruge kaenda Taifa linahuzunika.

“Kama shida ni figo ungeniambia nikupe yangu, wazazi wangu walifariki Ruge ndio alikuwa Baba na ndio mama, Watoto wengi unawaoona THT wametoka kwenye maisha ya shida Ruge alikuwa ndio Baba yetu” BarnabaClassic.

“Leo niko hapa nikiwa na Ujasiri niliojazwa na #JasiriMuongozaNjia…kwa sababu ya yale maono ambayo aliniambia….nasimama kama Mbunge” Professor Jay.

Professor Jay anasema alikutana na #RugeMutahaba mwaka 1999 siku ambayo walikuwa wanarekodi #ChemshaBongo. Ruge aliingia studio akiwa Joseph Kusaga na marehemu Brenda Fassie wa Afrika Kusini.

Ruge alisikia ile ngoma, (Chemsha Bongo) akausimamia na kuufanya mkubwa. Huo ndio wimbo uliofanya mapinduzi makubwa kwani ulikuwa na mawazo chanya ambayo hayakutarajiwa kusikika kwenye #BongoFleva.

JANUARY MAKAMBA AMUOMBA RUGE AMUONYESHE ISHARA: TUFANYE NINI? “Majonzi yangu ni kwamba umeondoka kabla sijalipa kwa ukamilifu deni langu kwako. Deni la upendo na urafiki wa kweli. Ulinipa heshima kubwa ya kuwa msiri wako – kwa kuniamini na kunielezea wasiwasi wako, ndoto zako, matumaini yako, harakati zako, mipango yako. Ulinipa heshima ya kunipa fursa ya kubishana nawe kuhusu mawazo na fikra zako.
Majonzi yangu ni kwamba kuna vitu fulani vikubwa na vizuri tulivipanga – mimi na marafiki na wadogo zako, kwa ajili yako, kwa staili yako – mapema mwezi Machi, ambavyo naamini vingekupa tabasamu. Kama unaweza, hapo ulipolala, TUPE ISHARA TUFANYEJE”

“Ruge hakuwa tajiri wa mali.. Ruge amebaki kuwa mtu mwenye moyo mpana wenye nafasi kwa kila mtu, kila wakati…na hiyo ndiyo Legacy yake”-January Makamba.

“Hatuwezi kumjengea #RugeMutahaba mnara utakaopambwa kwa chokaa, kwa sababu ameshajijengea mnara mioyoni mwetu. Mnara ambao hautaharibiwa na mvua, mnara ambao hauwezi kuvunjika.” Waziri Mwakyembe.

Ommy Dimpoz alivyokuja kwenye XXL alisema anaamini Ruge Mutahaba atasimama tena na kurudi kwenye majukumu yake, lakini imekuwa tofauti, machozi ya uchungu yanamtoka kwani tumaini lake limekuwa tofauti.

#JasiriMuongozaNjia

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here