Home Kitaifa Mafanikio ya Simba kimataifa vilabu vikubwa vyampapatikia Aussems

Mafanikio ya Simba kimataifa vilabu vikubwa vyampapatikia Aussems

6867
0

Mafanikio ya Simba chini ya kocha Patrick Aussems yameanza kuvipagawisha vilabu kadha wa kadha barani Afrika ambavyo baadhi tayari vimeanza kutuma offer vikitaka huduma ya Aussems maarufu Bongo kwa jina la UCHEBE.

Ikiwa ni msimu wake wa kwanza, Aussema amefanikiwa kuisaidia Simba kutinga hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa Afrika ambapo Simba ilikuwa haijafuzu hatua hiyo kwa muda mrefu (miaka 15) pamoja na kushinda mechi dhidi ya vigogo vya Afrika Al Ahly na JS Saoura vilabu vingi vikubwa vya Afrika vimeanza kumfuatilia Aussems.

Wakala wa Aussems Bw. Faustino Mukandila amesema baada ya mteja wake kupata mafanikio kwa muda mfupi kwenye mashindano ya kimataifa, ameanza kutafutwa na baahi ya vilabu vikitaka huduma ya Aussems.

“Kabla ya kuja Simba kuna vilabu kadhaa vilikuwa vinavutiwa naye, tulifuatwa na Al-Merrikh ya Sudan lakini haikuwa chaguo lake. Na tunavyozunguza sasa hivi, kuna vilabu vya Algeria, Morocco, Libya, Congo DR, Misri pamoja na timu moja kubwa ya Kenya vinamuulizia baada ya Simba kufanya vizuri kwenye mashindano ya Afrika”-Faustino Mukandila, wakala wa kocha Patrick Aussems.

“Mimi na Patrick tunafahamu namna ya kufanya kazi, sio siri kila mmoja anafahamu Patrick anafurahi kufanya kazi Simba. Ni mtu ambaye anapenda kufanya kazi sehemu moja kwa muda mrefu kama ilivyokuwa Benin. Kwa hiyo hatuwezi kulazimisha kuondoka wakati Simba wanajua nini tunataka na Patrick yupo tayari kuendelea kubaki Simba.”

“Ni juu yao wenyewe (Simba) kuja kwetu tuzungumze kinyume na hapo kocha atafanya kazi kwa nguvu zake zote hadi mkataba wake wa mwaka mmoja utakapomalizika halafu tutaangalia nini cha kufanya.”

Aussems amewahi kuwa kocha wa timu ya taifa ya Benin kwa miaka mitatu mfululizo.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here