Home Kimataifa Madili haya ni “Pasua Kichwa”

Madili haya ni “Pasua Kichwa”

12515
0

Makocha na mashabiki wengi huwa wanakosa sana amani wakati wa usajili. Ukisikia mchezaji wako anahitajika na vilabu kama PSG, Real Madrid, Barcelona na Man United basi matumbo joto. Kwa sasa kuna baadhi ya sajili zimeshika sana hatamu. Baadhi ya wachezaji wanahitajika kwa gharama yeyote na vilabu husika havitaki kuwaachia wachezaji wake hao waende.

Hazard Eden thamani 💶 Milioni 200

Kocha mkuu wa Chelsea Maurizio Sarri hataki kumuachia Hazard. Madrid inamhitaji ili kuziba pengo la Ronaldo Barcelona pia wanaleta kivuli kuonesha nia ya kumhitaji na hii ndio sababu kubwa hasa ya kupanda kwa thamani kwa hazard. Anahitajika ndani ya pembe 3, (Cjelsea, Madrid, na Barcelona)

Uwezekano wa kuondoka (100%)

Madrid wana asilimia 30 ya kumpata kwa sababu hawaogopi kutumia hela na huyo ndiye mbadala sahihi zaidi.

Barcelona wana asilimia 25 ya kumpata kutokana na ubora na ukubwa wa klabu hiyo. Wapo nyuma asilimia 5 ya Madrid kwani Hazard anaweza akatazama uwezekano wa kupata nafasi ya uhakika Barcelona zaidi, na anaweza kuamua kwenda Madrid ambapo ana uwezo wa kuwa nyota wa timu tofauti na Barcelona nyota wa timu ni Messi.

Chelsea wana asilimia 45 za kumbakiza. Hazard hana wenge na ni mmoja kati ya wachezaji watulivu. Pia anaipenda sana Chelsea na sio mchezaji anayeonesha tamaa. Chelsea pia dau waliloweka ni kubwa mno.

Maguire Harry thamani 💶 milioni 65

Leicester ni wabishi na ipo kwenye wakati mgumu wa kupoteza baadhi ya nyota wake muhimu. Alianza N’golo Kante kwenda Chelsea, Drinkwater Danny pia, na msimu huu Riyadh Mahrez ameleekea Man City. Harry Maguire anahitajika kwa udi na uvumba ndani ya klabu Man United. Jose Mourinho anataka kushindana vyema msimu ujao. Liverpool na Man City pamoja na klabu zingine zimefanya usajili mkubwa. United mpaka sasa hakuna usajili mkubwa uliofanyika utakaotishia vilabu vikubwa na kuleta hofu.

Uwezekano wa kusajiliwa (100%)

Man United ina uhakika wa kumpata kwa asilimia 60. Kwanza wana hela nyingi na wamekwisha kujitahatadharisha kutokana na usajili unaofanyika kwingineko.

Real Madrid wana asilimia 10 tu kutokana na kwamba hawajaweka sana nia maana kikosi chao ni imara na Maguire ni ngumu kuchukua uamuzi wa kwenda Bernabeu kutokana na ufinyu wa nafasi.

Leicester wana asilimia 30 tu ya kumbakiza kutokana na nguvu ya hela na istoshe Maguire pia hawezi kukataa ofa ya timu kubwa kama United. Kocha wa Leicester City Claude Puel, amesisitiza tena imani yake kwamba, mchezaji wake Harry Maguire, mwenye umri wa miaka 25, atasalia katika klabu yake ya Leicester, licha ya kuhusishwa kujiunga na Manchester United.

Anthony Martial thamani 💶 milioni 70

Mourinho hamtaki Martial, Martial hamtaki Mourinho, Man united inamtaka Martial. Ni ngumu sana kwa bodi ya United kumwachia mchezaji mchanga mwenye kipaji kama yule eti kisa tu mwalimu haendani na falsafa zake.

Uwezekano wa kuondoka (100%)

50 kwa 50 kuondoka au kubaki. Kwa sababu tayari Martial haoneshi moyo wake tena kwa United. Ed Woodward anaweza kumbakiza kwa sababu tu anahisi huenda Mourinho akaondoka na wakafanikiwa kumtumia vyema Martial hapo baadae.

Wanakumbuka sana yaliyowatokea kwa Pogba hivyo ni ngumu wao kurudia kosa.

Christian Pulisic thamani 💶 Milioni 60

Hivi majuzi Borussia Dotmund walijitahidi kweli kumuomba Pulisic asaini mkataba mpya lakini aligoma. Hayupo tayari kubakia klabu hapo. Klabu yake imeweka dau kubwa mno. Cheslea wapo tayari kumchukua lakini dili lake nalo litategemeana na dili lingine kichaa la Willian kwenda Barcelona au Man United.

Barcelona inamuwinda Wilian licha ya kwamba hawajapelela ofa yeyote. Ofa ya Willian ndiyo iyakayoamua kumtwaa Pulisic. Hata hivyo BVB wamesema hiyo bei wameshusha kwa muda tu. Wanaamini kuwa thamani yake ni kubwa zaidi.

Uwezekano wa kuondoka (100%)

Hili nalo ni 50 kwa 50. Chelsea wanategemea hela ya kibati ili kumpata. Yeye mwenyewe anahitaji kuondoka. Ni kama mbuzi kafia kwa muuza supu maana yeye mwenyewe anasaka nafasi ya kucheza klabu kubwa.

Wilian & Hazard Thamani 💶 Milioni 300
Dili la mmoja wao ndilo litakaloua la mwenzake. Sidhani kaa hawa wote wanaweza kjondoka kwa wakati mmoja. Kama Wilian ataenda Barcelona basi Madrid hawasahau kuhusu Hazard. Kama Hazard ataenda Madrid kuna ukakasi sana wa Wilian kuondoka hapo.

Kwanza Chelsea watakuwa na Milion 200 mfukoni, Pulisic anapatikana kwa Euro Milion 60 bado watabakiwa na milion 140 + Willian hivyo wanaweza kununua wachezaji wengine kama vile Martial Milion 70 n.k

Uwezekano wa wote kuondoka 10%
Uwezekano wa mmoja kuondoka 70%
Uwezekano wa wote kubaki 5%

Lewandowski thamani haijajulikana

Huyu tokea msimu uishe yeye anatangaza kuhama tu. hatujasikia taafifa zinzomhusisha kuondoka. Kocha mkuu wa Bayern amesema haondoki wakala anasema anaondoka.

Uwezekano wa kuondoka 50/50%

Usiache kufuatilia ukurasa wetu huu kila saa kujua yanayotokea masokoni, Instagram na facebook Shaffih dauda, Mimi ni Privaldinho (Instagram)

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here