Home Kimataifa Mabeki wa Arsenal wana kiwewe

Mabeki wa Arsenal wana kiwewe

4710
0

Unai Emery, ni moja ya makocha wazuri Barani Ulaya, kwa sasa anaifundisha klabu ya Arsenal, katika ligi kuu England ndo Kwanza msimu wake wa Kwanza tumeona mapinduzi katika klabu hiyo wachezaji wengi ni wale wale ukiwatoa Torreira, Guendozi ndo aliyowaongeza katika idara ya Kiungo.Arsenal, ina tatizo katika idara ya ulinzi hili tatizo pengine ndo limekuwa likimsumbua sana Unai.Mechi nyingi anazocheza amekuwa hakai chini kwa sababu presha na kuwakumbusha mabeki wake majukumu ndani ya uwanja.Msimu huu Arsenal, katika idara hiyo imekuwa aina Consistency nzuri (muendelezo mzuri) ukiangalia katika idara hiyo Mustafi, Holding, Sokratais,ni aina ya mabeki wazuri pale wanapokuwa na mpira kwa maana ya kuanzisha mashambulizi ndo wazuri zaidi.Katika idara ya kufanya marking (kukaba) hawana spidi na maamuzi kila siku mwalimu amekuwa akifanya mabadiliko katika idara hiyo kutafuta mtu muhimu lakini inakuwa ngumu.Safu hiyo wanapokutana na timu infanya mashambulizi ya kushutikiza kwa mpira mirefu wamekuwa wanakatika sana na kufanya makosa ambayo inawapa faida timu pinzani.Kochienly, umri umeenda kasi imepungua inahitaji ingie sokoni isajili beki mzuri ambaye ataweza kuwa kiongozi kuwaongoza wengine katika idara hiyo ukiangalia Liverpool, kuna Van Djick, City kuna LaPorte Chelsea kuna Luiz, tunaona kabisa Arsenal, tatizo kubwa katika idara hiyo.Mpaka sasa kwenye ligi kuu Arsenal, wameruhusu mabao 32 ni magoli mengine sana wameruhusu pengine hii itaweza kuwaletea shida zaidi.Arsenal, inateseka sana katika idara ya ulinzi majeraha mara kwa mara.Azizi _Mtambo_15

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here