Home Ligi EPL LVG KOCHA NYUNDO ANAYEAMINI KILA MCHEZAJI NI MSUMALI NA MBINU ZAKE ZA...

LVG KOCHA NYUNDO ANAYEAMINI KILA MCHEZAJI NI MSUMALI NA MBINU ZAKE ZA KIMIUJIZA

833
0

Van Gaal 4

Na David Wambura

Ulimuona Van Gaal na mbinu zake dhidi ya Spurs? Umewahi muona Juan Mata mchezaji ambaye kutokana na kukosa kwake uwezo wa kusaidia ulinzi wakati  tmu yake inashambuliwa kulimfanya Jose Mourinho kocha wa  Chelsea wakti huo alilazimika kumuondoa kwenye kikosi chake licha ya kuwa mchezaji bora wa klabu kwa miaka miwili mfurulizo. Mta huyo LVG alimuona anafaa kucheza fullback wa uongo (Auxiliary fullback) dhidi ya timu ya Spurs iliyo kwenye form, kila mtu hata mwenye uelewa mdogo kiasi gani wa soka angeweza kuyaona mapungufu hayo ya Mata, naamini hata Mata mwenyewe anayajua mapungufu yake hayo isipokua Van Gaal pekee.

LVG hana tofauti sana na nyundo, nyundo inaamini kila kitu ni msumali na kwamba mbele yake (nyundo) hakuna mahala msumali haupiti, LVG kama nyundo anaamini kila mchezaji chini yake anaweza cheza popote na kutimiza majukumu yake kikamilifu bila shida, kitu ambacho si sahihi mara zote.

Kwa mfano kwenye game dhidi ya Spurs, Juan Mata (central attacking midfielder-CAM) ambaye kwa kawaida hucheza kwenye shimo namba kumi alicheza kama full back wa uongo huku Fosu Mensah aliyepaswa kucheza fullback akipewa maelekezo ya kuingia ndani kumfuata Erick Lamela ambae alikua hakai pembeni anaingia katikati, hiyo ilimfanya Mata mara nyingi kuwa anakutana mmoja dhidi ya mmoja na Danny Rose.

Lingard ambaye kwa kawaida hucheza kama mshambuliaji wa kulia kati ya washambuliaji watatu wa mbele alipangwa mahala pa kawaida pa Mata (namba kumi),  bumbuwazi lilizidi zaidi baada ya Ashley Young kuchukua nafasi ya Marcus Rashford na kucheza namba tisa wa uongo (Auxiliary number nine) badala ya wengi tulivyodhani angebadilishana namba na Martial, Young aende pembeni Martial arudi katikati.

Sasa sio kwamba hizo ‘awkward tactics’ zake hazikuwa na maana kabisa jibu ni hapana kulikua na maana fulani ila shida wachezaji hawakua huru kwenye maeneo waliyopangwa kutokana na kutoyazoea. Kwa mfano lengo la kumpa maelekezo Fosu Mensah aingie ndani zaidi ilkua kujaribu kutafuta uwiano wa idadi ya wachezaji kati ya Spurs na timu yake sababu kwa Lamela kuinngia mara nyingi katikati kuliwafanya Spurs kuwa wengi katikati hivyo Mensah alitumika kama mtu wa ziada kuweka uwiano sawa.

Wakati kumchezesha Lingard namba kumi na Ashley Young namba tisa lengo lake lilikua kujiarbu kuwa na watu wengi wenye mbio nyuma ya midfield na defense ya Spurs(free runners) lakini pia alijaribu kuwatengenezea tatizo mabeki wa kati wa Spurs tatizo ambalo hawajalizoea. Tunajua mabeki wa kati wamezoea kuwa na na watu wa kuwa mark lakini kwa kutokuwa na namba tisa anayesimama kwenye box maana yake ni kwamba  mabeki wa Spurs wasingejua nani wa kum-mark. Lakini kama nilivyosema hapo juu wachezaji hawakua confortable kwenye maeneo na majukumu yao mapya hususan Juan Mata.

Lakini swali la pili la kujiuliza ni je hakukuwa na namna nyingne ya kuwadhibiti Spurs bila kuwalazimisha wachezaji kuwa misumali? Kwa mfano badala ya kumuingiza Mensah ndani kila mara angeweza kuongeza kiungo mmoja na kupunguza  mshambuliaji mmoja mfano angeweza wachezesha Morgan, Carrick na Ander Herrera huku Mata au Lingard akicheza kama mshmbuliaji wa kulia, Martial katikati na Ashley Young akitokea kushoto, au hata Mata akacheza juu ya Morgan na Carrick huku huko kwingne wakiendelea kuwa kama walivyo kwa kufanya hivyo angeweza kupata alichokitaka kwenye timu yake na kuwadhibiti Spurs na kuzuia faida ya mtu wa ziada waliyokuwanayo Spurs kila walipokuwa wanashambulia na hivyo kuweka uwiano sawa kati ya wachezji wao na wale wa Spurs.
Lakini kingne chakuchekesha zaidi hii haikuwa mara ya kwanza LVG kutumi mbinu kama hiyo, muda si mrefu  sana aliitumia mbinu kama hiyo dhidi ya Liverpool Anfield kwenye Europa League, tofauti tu ni kwamba badala ya Mata kucheza kama fullback wa uongo mahala hapo alicheza Marcus Rashford huku Guilermo Varela akipewa jukumu la kutembea na Phelipe Coutinho aliyekua anaingia katikati mara nyingi na kitendo hicho  kilimfanya Rashford kukutana mara kwa mara mmoja dhidi ya mmoja na Alberto Moreno.

Kinachokitisha zaidi ni kwamba, unawezaje tumia mbinu mbaya ikapelekea matokeo na kiwango kibovu kwenye moja ya mechi muhimu za msimu lakini bado ukawa ma imani na ujasri wa kuizitumia tena mbinu hizohizo kwenye mechi yenye uzito sawa na wa mwanzo? Kwa kufanya hivyo LVG ali-vindicate msemo maarufu uliowahi tumika na ambao unatumika sana hadi leo kwamba “uwendawazimu ni kutumia njia zilezile kwa style ileile ukitegemea matokeo tofauti” ‘insanity is keep on doing the same thing the same way while expecting different results’.

LVG yawezekana ulichofanya kilileta maana kwako na kwamba ungepata matokeo ungeonekana genius bahati mbaya ni kwamba hilo hailikutokea mechi zote na sasa kila mpenda soka ana kibali cha kukuita ‘mwendawazimu’, kitu ambacho naamini hata Giggs msaidizi wako alikifanya kimoyomoyo baada ya mechi kuisha, sura yake ilionyesha hivyo. Ushauri wangu kwako ni rahisi tu na nakupa bure kabisa hebu usifikirie sana, mpira ni mchezo rahisi tu ila wewe umeufanya kama mtihani wa Physics form six, wenye timu yao hawakuelewi, wamechoka na sasa wanataka ‘ama kichwa chako ama damu yako’.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here