Home Uncategorized Lord Jesse Lingard aliwahi kupigwa na Fergie

Lord Jesse Lingard aliwahi kupigwa na Fergie

5831
0

Jana Lingard aliwafanya vibaya sana Arsenal FC baada ya kuwapiga bao lake la 3 dhidi yao. Lingard amebadilika kwa kiasi kikubwa sana.

Wengi tumekuwa tumedharau sana hasa kwa kuwa sio mchezaji mwenye maamuzi ya haraka sana, lakini jitihada zake na hari ya upambanaji inamshawishi mwalimu yeyote kumpanga.

Lingard anadai pia miaka kadhaa akiwa kijana mdogo aliwahi kukumbana na hasira za kocha mwenye mafanikio makubwa sana katika klabu hiyo Sir Alex Ferguson.

“Nilitoka mazoezini nikawa napita kwenye korido za Man United nikiwa naburuza mguu huku nikipiga makelele”

“Wakati napita upande wa pili kocha alikuwa akitoa maelezo kwa timu ya wakubwa”

“Ghafla nikapigwa kiatu cha kichwa. Nikageuka kwa haraka na gadhabu nikakutana nae akiwa amefura hasira”

“(We kijana kwanini unatabia chafu. Unasumbua kaka zako nani kakufundisha huo upuuzi Shenzi kabisa), Nikanywea kama nimemwagiwa maji ya baridi”

“Sikuweza kumjibu niliondoka zangu taaratibu maana kama ningemgeuza kidogo nahisi ningekula vibao” Alisema Lingard

Lingard pia aliongeza kuwa mtu pekee aliyemfanya asiondoke Old Traffird ni kocha huyo Fergie

“Nilipokuwa mdogo niliona wachezaji wengi wakipewa mikataba lakini mimi holaa”

“Siku moja nikiwa na miaka 16 aliniita mimi na familia yangu kwenye ofisi yake.

Akaniambia

“Lingard una kipaji kizuri lakini kuwa mvumilivu muda bado. Nitakupandisha kikosi cha kwanza ukiwa na miaka 22 au 23.”


Nadhani wengi wanapaswa kujifunza kupita Lingard akiwa na miaka 16 anaambiwa utacheza miaka 7 ijayo. Kikawaida wachezaji wengi sio wavumilivu, hukimbia au kwenda kucheza vilabu vingine kwa kuhofia kuwa muda ni mrefu.

Lakini uvumilivu wa Lingard umenfanya sasa awe mmoja kati ya wachezaji muhimu sana

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here