Home Ligi EPL Liverpool kwa Allison Becker safi lakini Chelsea kwa hu Kepa hapana aisee...

Liverpool kwa Allison Becker safi lakini Chelsea kwa hu Kepa hapana aisee mmeibiwa!

18926
0

Kocha wa Manchester United Jose Mourinho wakati United wakimnunua Pogba alishambuliwa sana kwa bei aliyomnunulia lakini baadae akasema ni jambo la kawaida sana na siku sio nyingi Pogba ataonekana alinunuliwa kwa pesa chache.

Baadaye Neymar akaenda PSG £195m zikimng’oa Barcelona watu wakaanza kuona namna ambavyo pesa imeanza kuwa na matumizi makubwa sana kwenye soka na pengine kuzidi hata thamani halisi ya wachezaji.

Allison Becker alipouzwa Liverpool kwa £67m watu walishtuka kwa kuwa ilionekana ghali, lakini Kepa Arrizabalaga kusaini Chelsea kwa £71m haichanganyi tu bali inaweza kukupa kizunguzungu ukabaki kujiuliza kwanini.

Binafsi sijawahi msikia Kepa akitajwa tajwa na kwa mawazo yangu baada ya Becker kwenda Liverpool kwa haraka haraka kipa ambaye nilimuona anaweza kuvunja rekodi yake ya usajili ukiacha De Gea(hanunuliki/hauzwi) ni mlinda lango wa Ac Milan Gianluigi Donnaruma lakini Kepa hapana aisee.

Kwa uzoefu Kepa hana uzoefu wa kiasi cha £71m, na sio mbaya kwa kuwa keshanunuliwa Chelsea na Becker kasaini Liverpool ni bora leo tuone uzoefu na ubora wa makipa hawa wawili.

Kepa Arrizabalaga. Balaga hajawahi kusajiliwa na timu nyingine toka ajiunge na Athletic Bilbao mwaka 2014 lakini ambacho kilitokea ni kwamba alikuwa hana nafasi katika kikosi hicho na akawa anatolewa tolewa kwa mkopo kupata uzoefu.

Lakini sasa Kepa hata timu ambazo alikuwa akitolewa kwa mkopo hazikuwa timu ambazo zinashiriki ligi kubwa hivyo uzoefu ameupata katika madaraja ya chini tu na sio katika ligi kubwa.

2011/2013 alitolewa kwa mkopo katika klabu ya Basconia ambayo ni kama ligi daraja la 3 nchini Hispania kabla ya kurudishwa tena Bilbao katika msimu wa mwaka 2014.

Akacheza mechi chache kisha Atletic Bilbao wakamtoa tena kwa mkopo katika timu nyingine daraja la chini iitwayo Ponferradina ambapo baada ya hapo akaenda tena kwa mkopo kwenye timu nyingine huko huko daraja la pili iitwayo Valladolid.

Msimu uliopita ambao Kepa alikuwa katika lango la Bilbao wamfungwa mabao 49 katika La Liga pekee, huku timu hiyo ikimaliza ligi katika nafasi ya 16(4 kutoka chini) bado kipa huyu kasajiliwa kwa rekodi ya dunia SMH.

Msimu uliopita amefanya saving 99 na clean sheets 7/38 ni saving nyingi lakini Kepa sio mchezaji wa kwanza kuwa na msimu mzuri mmoja na kisha akapotea (one season wonder) tuna uhakika gani kwamba huyu sio one season wonder?

Kuna mambo mawili nayaona kwenye usajili wa Kepa, moja ni labda Chelsea wako na stress baada ya Courtouis kulazimisha kuondoka wakawa wako tayari kufanya lolote kumnunua mziba pengo wa Courtois ndio maana wakatoa kiasi hicho cha pesa.

Lakini pili Chelsea hawapo Champions League, wapo katika michuano ya Europa na pengine wanaona ni bora kumuamini Kepa kwa kipindi hichi na kumpa uzoefu ili hata mwakani wakifanikiwa kurudi Champions League awe ameimarika.

Allison Becker(Liverpool). Allison Becker kabla hata Liverpool hawajampoint tayari alikuwa kati ya makipa ambao wanazungumziwa sana kutokana na uzoefu wake katika timu ya taifa na klabu.

Sport Club Internacional. Ukubwa wa Allison Becker ulianzia hapa mwaka 2013 na kama haujui tu Becker ndiye alimpoteza mlinda lango wa zamani wa Brazil Dida ambaye walikuwa wakiwania namba katika klabu hiyo ya Internacional.

Dida wakati akihamia Intenational toka Gremio alimkuta Becker na hapo ndipo Dida alisugua benchi na Becker akafanikiwa kuwa kipa namba moja Internacional akicheza mechi 100 (michuano yote) huku zote akibeba kombe.

As Roma. August mwaka 2017 As Roma walianza kumtumia Becker na hii ilikuwa Champions League wakisuluhu bao 1-1 dhidi ya Porto,lakini tofauti na alikotoka akawa kipa namba mbili As Roma nyuma ya Wojciech Szczesny.

Baadae Szczesny aliachana na As Roma na kuhamia Juventus ndipo Becker alipoanza kupewa nafasi ,alikuwepo katika kikosi cha Roma ambacho hakikuwahi kuruhusu bao katika uwanja wao wa Stadio Olimpico katika UEFA hadi siku wamefungwa na Liverpool.

Katika misimu ambayo Becker amekaa Roma amecheza Serie A, Champions League kwa muda na huku akiwa na clean sheets 22 kati ya hizo kuna 17 katika ligi na ana clean sheets 5 UEFA.

Brazil. Kabla hata ya kwenda Urusi, Allison Becker alikuwepo katika safari ya Brazil kwenda Urusi akicheza mechi 16 za kufudhu katika michuano hiyo, lakini May 18 mwaka jana alitajwa katika katika kikosi cha timu ya taifa ya Brazil iliyoenda Urusi kombe la dunia.

Swali, kama Kepa golikipa ambaye hana udhoefu na michuano yoyote mikubwa nje ya Hispania, hajawahi cheza champions league, timu yake imemaliza nafasi ya 16 La Liga, timu ya taifa kacheza mechi 1 na anauzwa £71m, je manguli kama Courtois, De Gea, Neur, Buffon watakuwa na thamani gani halisi kwa kile wanachoionesha dunia?

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here