Home Ligi BUNDESLIGA VIDEO- LEWANDOWSKI AFUNGA BAYERN IKISHINDA UGENINI BUNDESLIGA

VIDEO- LEWANDOWSKI AFUNGA BAYERN IKISHINDA UGENINI BUNDESLIGA

966
0

lewaRobert Lewandowski alifunga goli lake la nne kwenye mechi mbili za Bundesliga na kuisaidia Bayern Munich kushinda ugenini dhidi ya Schalke 04.

Mabingwa hao wa Ujerumani mapema kabisa walionekana kama wamekata tamaa baada ya mshambuliaji wao tegemezi Lewandowski kukosa goli kwenye eneo la sita.

Lakini baadaye aliifuta makosa yake baada ya kufunga goli murua dakika ya 81 kufuatia pasi nzuri kutoka kwa Javier Martinez na kutoa tena pasi ya goli la pili lililofungwa na Joshua Kimmich.

Mshambuliaji wa Schalke Klaas-Jan Huntelaar alikarabia kufunga lakini mpira wake uligonga mwamba wakati huo timu zote zikiwa hazijafungana.

Mchezaji aliyetokea benchi Kimmich, 21, amefunga leo baada ya kutoka kuifungia timu yake ya Ujerumani kwenye ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Norway kwenye mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia mwaka 2018 nchini Russia. Goli lake kwenye mchezo huu ni la kwanza tangu aichezee Bayern.

Kiungo wa Bayern Renato Sanches (19), ambaye aliisaidia Ureno kushinda ubingwa wa Euro Euro 2016, alikuwa akicheza mchezo wake wa kwanza kwenye ligi ya Bundesliga baada ya kusajiliwa kwenye dirisha la majira ya kiangazi akitokea Benfica.

Mpaka sasa Bayern wamefikisha alama sita chini ya meneja wao Carlo Ancelotti kufuatia kushinda michezo yao yote miwili.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here