Home Kimataifa Lebron James ahamia Lakers kwa mkataba mkubwa zaidi NBA – Amkalisha Curry

Lebron James ahamia Lakers kwa mkataba mkubwa zaidi NBA – Amkalisha Curry

10216
0

Baada ya kizungumkuti cha wapi ataelekea kucheza msimu ujao hatimaye Lebron James ameamua kuhamishia maisha yake magharibi mwa pwani ya Marekani – Los Angeles.

James ataanza kuitumikia timu ya mpira wa kikapu ya Los Angeles Lakers kuanzia msimu ujao kwa mkataba wa miaka 4 wenye thamani ya $154m.

Mkataba huu umetangazwa kupitia wakala wake kampuni ya Klutch Sports Group, baada ya siku nzima ya jana kuwepo na tetesi nyingi kwamba anaelekea LA Lakers.

Mkataba huu ambao ndio mrefu kuliko yote amabyo amewahi kusaini Lebron tangu aliposaini mkataba wa miaka 6 na Miami Heat mwaka 2010 – unamfanya Lebron kuwa mchezaji anayelipwa fedha nyingi zaidi katika NBA.

Lebron James msimu uliopita akiwa anaitumikia Cleveland Carvaliers alilipwa mshahara pekee wa $33m wakati akimalizia mkataba wa miaka 3, alishika nafasi ya pili katika wachezaji wanaolipwa fedha nyingi katika NBA – huku Stephen Curry akikamata usukani kwa dili la miaka 5 na Golden State Warriors akilipwa mshahara wa $34m kwa mwaka.

Kwa mkataba wa huu sasa ina maana Lebron James atakuwa akienda bank akicheka kwa kulipwa $38m kwa mwaka – dili linalomfanya awe mchezaji anayelipwa fedha nyingi za mshahara katika NBA.

Mchanganuo wa malipo mapya ya Lebron James

$154,000,000 ÷ 4 miaka = $38.5M – malipo ya mwaka

$38,500,000 ÷ 12= $3.20m ( Billion 8 kwa mwezi

$3,208,333 ÷ 4 = $802,083 ( Zaidi ya Billioni 1.6 kwa wiki)

$822,500 ÷7= $117,500 (zaidi ya millioni 268 kwa siku)

$117,500 ÷ 24= $4,869 (Zaidi ya millioni 11 kwa saa 1)

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here