Home DOKUMENTARI La Masia ni kinyago cha Barcelona, hakina madhara tena

La Masia ni kinyago cha Barcelona, hakina madhara tena

13422
0

Ukiitazamana kwa makini NOU CAMP utagundua inaangamia taratibu ikiwa na tai shingoni. Wanahaha kila kukicha. Hivi majuzi kuna watu waliikebehi Barcelona kuwa imegeuka kuwa Madridfication kwa wale wajuvi wa kiingereza mtusaidie

Johan Cruyff alipowasilia Barcelona 1973 hakuna mtu aliyejua kama ataleta mapinduzi makubwa ya soka kwa klabu ile.

Cruyff alitambulisha mfumo wa soka safi, soka la akili na ufundi zaidi. Hakuhitaji vifaa vizuri vya gym wala wachezaji kuteseka juani. Alikataa katukatu mpira wa madoido kama wabrazil na kupuuza mpira wa nguvu kama wajerumani.

Alishauri kuwa ili mfumo ule ufanye kazi vyema ni lazima uanzishwe kwenye kizazi cha ukuaji cha vijana wadogo kabisa wa Barcelona B na wale wa La Masia. Akaja na mfumo wa tiki-taka pasi kama zote.

Kutoka mwaka 1979 – 2009, vijana 440 wamekimbia majumbani kwao na kwenda kujiunga kwenye jumba la La Masia. Nusu yao wengi walitokea Catalonia, wengine walitokea Himaya ya Hispania, vijana 15 kutoka Cameroon, 7 kutoka Brazil, 5 kutoka Senegal na 3 kutoka Argentina. Kati ya hao 440, ni 40 waliofanikiwa kuingia kikosi cha kwanza cha Barcelona.

Wachezaji takribani 7 walishiriki fainali ya UEFA mwaka 2011 walitpkea La Masia. Mpaka sasa hakuna mchezaji aliyefanikiwa kujipatia nafasi katika kikosi hicho. Amekuja Serge Roberto ambaye ameletewa Nelson Semedo.

Leo hii La Masia imeshindwa kabisa kuilisha Barcelona B na Barcelona kubwa wachezaji wazuri mwisho wa siku imeshushwa daraja chini ya mkufunzi Xavi García Pimienta na Barcelona B imeelekea Segunda Division B.

Msimu Ligi Daraja No
2010–11 2 3rd
2011–12 2 8th
2012–13 2 9th
2013–14 2 3rd
2014–15 2 22nd
2015–16 3 2ª B 10th
2016–17 3 2ª B 1st
2017–18 2 20th
2018–19 3 2ª B

La Masia ya Johan Cruyff imeshakufa sasa imebaki jina tu. Hawana jipya. Sawa tumeona wachezaji wazuri kama Xavi Simmons lakini limebaki lile jengo kubwa lisilo na mwelekeo wowote.

Kilichoiangamiza La Masia ni ukiukwaji wa maadili yaliyowekwa na Cruyff. Barcelona imeachana na utamaduni wake wa hapo awali. Filamu lilianzia kwa Neymar na Luis Suarez ambao wote waligharimu €168 million. Kweli Barcelona ni ya kuwekeza zaidi ya milioni 100 kwa mchezaji ambaye hakuwahi kupata nafasi timu ya taifa? (Dembele)

Ujio wa Paulinho na Dembele kuzba nafasi ya Neymar ni dalili mbaya kwa La Masia. Gerard Pique mwenyewe anakiri kuwa Barcelona inadondoka. Iko wapi Barcelona iliyomtetemesha Fergie vidole?

Yule ambaye Tottenham ilimuona flopu Paulinho wao wakamwaga zaidi ya £36.4m ili kumnasa. Na kweli akageuka kuwa mkombozi wao. Hii ni dalili mbaya kabisa kwa La Masia.

Ameondoka Alcantara, akafuata Fabregas, kisha Xavi sasa tumemaliza na Iniesta. Wenye uhai ni Sergio Busquets, Lionel Messi, Pique na Sergi Roberto. Hakuna ingizo jipya. Kwanza ndo Barcelona wanahangaika na akina Pogba na Hazard pamoja na Willian. Ni juzi juzi tu wametoa Milion 120 kwa ajili ya Coutinho na 120 kwa ajili ya Dembele. Wameleta Athur na Malcom wote kwa gharama kubwa kubwa. Sasa unajiuliza ile La Masia tishio imeishia wapi?

Tatizo kubwa ni Josep Bartomeu pamoja na bodi yake yote.

Uwajibikaji na kujitoa kwa viongozi wa Barcelona kwa upande wa La Masia umekuwa mdogo sana imefika kipindi hadi mashabiki wanalalamika. Klabu inapoteza ladha, heshima na makali yake.

Ukitaka kujua kifo cha mke ndicho kinachosababisha mume ateseke kitandani, angalia walivyonyanyasika kwa As roma. Ni Barcelona ile ile yenye mchezaji bora wa dunia mara tano iliduwazwa. Kwanini? Kwa ssababu waliusaliti mfumo wao waliotoka nao  chini La Masia, au La Masia de Can Planes. Mfumo wa Barcelona kushnei. Hakuna tena zile pasi 1000. Hakuna tena wale vichaa Xavi na Iniesta.

Kifo cha La Masia kimeiangamiza Barcelona.

Alikuja Gerard Deulofeu ambaye wengi walimsifu moja ya vipaji maridhawa tokea Messi kutoka La Masia.

Mpaka anafikisha miaka 22 ameishi kama mkimbizi ndani ya Camp Nou. Alienda kwa mkopo Everton, pia akatimkia Sevilla kwa mkopo, kabla hajarudi tena Everton moja kwa moja. Pale Upton Park penyewe amekosa nafasi na sasa amelekea AC Milan kwa mkopo.

La Masia wanatoa vyeti feki tu kwa sasa. Deulofeu bado ni mdogo lakini ni dhambi kusema kuwa yeye ndiye mchezaji bora zaidi kutokea La Masia tokea Messi kama wengi walivyompachika wakati anatokea pale.

Sio Deulofeu pekee pia wapo Bojan Krkic, Adama Traore, Sandro Ramirez, Marc Bartra, Cristian Tello, Isaac Cuenca, Thiago Alcantara na wengineo wachanga waliopotelea mchangani.

Inawezekana Roberto ndiye mchezaji pekee aliyedumu kikosini Barcelona kwa kipindi cha hivi karibuni.

Hili kundi la akina Jordi Alba na Denis Suarez hatuwezi kusema kuwa moja kwa moja wametokea La Masia kwa sababu kabla ya kupata nafasi waliuzwa kisha wakarudishwa tena.

Hatuwezi kusema kuwa La Masia sio kitu.

Hapana. Mafanikio makubwa ya Barcelona ni La Masia. Kizazi cha Xavi Hernandez, Andres Iniesta, Pedro, Busquets na Messi hakiwezi kupuuzwa hata kwa makusudi.

Uhuni na tamaa uliitawala sana La Masia.

Unakumbuka sakata la uchunguzi wa FIFA la kuchukua wachezaji wa U-18 wa kimataifa? Barcelona ikagundulika kuwa wachezaji 10 walisajiliwa kinyume cha sheria za FIFA. Ndani ya miaka miwili heshima ya Barca ikavuja. Heshima ya Rais Sandro Rosell kisha Josep Bartomeu kuchukua hatamu.

Ndani ya miaka miwili La Masia ikapoteza wachezaji wazuri kabisa ambao hapo kesho itajutia sana.

Andre Onana (Ajax), Bobby Adekanye (Liverpool), Maudo Diallo (Roma) na Javi Romero (Sevilla). Hivi karibuni pia imewapoteza Eric Garcia (Manchester City), Adrian Bernabe (Manchester City), Sergio Gomez, (Borussia Dortmund), Kays Ruiz-Atil (PSG), Robert Navarro (AS Monaco) na Jordi Mboula (AS Monaco)

Wote wameondoka na kwenda kwenye akademi zingine baada ya kuona La Masia ni miyeyusho.

 

Katika kipindi chote hicho Barcelona wanateseka Madrid wametwaa UEFA mara 4 ikiwa na rekodi ya kutwaa mara 3 mfululizo

Wachezaji wa La Masia waliowahi kucheza zaidi ya michezo 100

Jina Utaifa Mwk M G
Xavi Spain 1998–2015 505 58
Andrés Iniesta Spain 2002– 2018 435 35
Lionel Messi Argen 2004– ¤ 414 378
Carles Puyol Spain 1999–2014 392 12
Víctor Valdés Spain 2002–2014 387 0
Guillermo Amor Spain 1988–1998 311 47
Sergio Busquets Spain 2008– ¤ 305 7
Gerard Piqué Spain 2008– ¤ 270 23
Sergi Barjuán Spain 1993–2002 267 6
Pep Guardiola Spain 1990–2001 263 6
Francisco Carrasco Spain 1978–1989 262 49
Tente Sánchez Spain 1976–1986 236 16
Cesc Fàbregas Spain 2011–2014 96 28
Pedro Spain 2007–2015 204 58
Albert Ferrer Spain 1990–1998 204 1
Antonio Olmo Spain 1976–1984 188 4
Jordi Alba Spain 2012– ¤ 155 6
Gabri García Spain 1999–2006 129 7
Oleguer Presas Spain 2001–2008 127 1
Sergi Roberto Spain 2010– ¤ 121 1
Ramón Calderé Spain 1984–1988 110 15
Bojan Krkić Spain 2007–2011

Mimi ni Privaldinho (Instagram)

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here