Home Kimataifa Kyrie Irving Akumbwa Na Mkosi, Giannis Antentokounmpo Mchezaji Bora NBA?

Kyrie Irving Akumbwa Na Mkosi, Giannis Antentokounmpo Mchezaji Bora NBA?

6043
0

Inawezekana jina la Giannis Antetokounmpo likawa maarufu kutokana na ugumu wake lakini tangu msimu uliopita amekuwa mchezaji anayetizamwa zaidi katika kundi la wachezaji vijana wanaoweza kuja kuitikisa NBA. Hii ndio sababu ambayo Kevin Durant alikiri kuwa Giannis ni mchezaji wa kipekee na anaweza kumaliza maisha ya NBA akiwa mchezaji bora zaidi kuwahi kutokea.

Alfajiri ya Leo, Giannis aliiongoza klabu yake ya Milwaukee Bucks kushinda mchezo wao wa kwanza dhidi ya Boston Celtics ambayo sasa itakuwa imepoteza michezo miwili mfululizo. Boston Celtics ambayo inaonekana kuwa na kikosi kipya kabisa kilichojaa vijana baada ya kuondokewa na nyota wake kama Isaiah Thomas, Avery Bradley, Jae Crowder na Kelly Olynyk imepoteza mchezo wake wa ili mfululizo huku ikiwa ni siku moja tangu kumpoteza nyota wao Gordon Hayward aliyevunjika vibaya dhidi ya Cleveland Cavaliers.

Giannis Antentokounmpo alifunga pointi 37 huku pia akidaka rebound 13, huku wenzie  Malcolm Brogdon akifunga pointi 19 na Khris Middleton akiongeza pointi 15 na kudaka rebounds 9 lakini pia Mathew Dellavedova alitoa mchango wake wa pointi 15 kwenye ushindi huo.

Kyrie Irving alikuwa na usiku atakaotaka kuusahau baada ya kumaliza mchezo na pointi 17 huku akipata mitupo 7 tu kati ya 25 aliyojaribu ikiwa ni mchezo wake wa kwanza nyumbani kwa Boston Celtics yaani TD Garden,  Jaylen Brown yeye aliongeza 18.

Kabla ya mchezo huo, kwenye screen maalumu ndani ya uwanja wa TD Garden, ilipita video ikimuonyesha Gordon akiwa hospitali akiwashukuru washabiki na wachezaji wenzie kwa kumtakia heri katika kuuguza majeraha.

HIGHLIGHTS

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here