Home Ligi EPL Kweli Pogba amekua, atoa sababu ya kutobadili nywele kombe la dunia

Kweli Pogba amekua, atoa sababu ya kutobadili nywele kombe la dunia

11012
0

Ufaransa walichukua ubingwa wa kombe la dunia na michezo yote ilipigwa huku kiungo wao “bishoo” Paul Pogba akicheza katika kiwango cha hali ya juu sana na kuwa moja ya chachu za Ufaransa kubeba ndoo.

Fomu ya Pogba kwa namna ilivyokuwa Urusi iliwashtua watu wengi na wengi wakimtaka Pogba huyo kwa kiwango hichohicho ndio akipeleke Manchester United.

Lakini kama ulimuona Pogba sio tu kiwango kilibadilika, ila hata kichwanu kwake kulikuwa na mabadiliko ya nywele zake, Pogba hakubadili style ya nywele zake hata mara moja.

Akiwa Manchester United amekuwa akibadili mitindo ya nywele karibia kila mechi, na kupaka karibia rangu zote kichwani mwake lakini akiwa na Ufaransa alibaki tu na nywele zake za kawaida.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram kuna shabiki alimuuliza Paul ni kwanini hakubadili mtindo wa nywele kwenye kombe la dunia?

Paul Pogba alimjibu shabiki huyo na kumuambia alitaka kuwa na amani na wekeze malengo yake katika soka tu na sio muonekano ili watu wamhukumu katika mpira tu sio vitu vingine.

Hii ina maana kubwa kwa Pogba kwani katika msimu uliopita EPL alikuwa akisemwa sana kuhusu kiwango na ubishoo haswa nywele zake, lakini anaonekana aliamua ni bora asemwe kuhusu kitu kimoja.

Haijafahamika moja kwa moja kwamba Pogba ataendelea kubadili nywele akiwa na Manchester United au atafanya kile alichofanya Urusi akiwa na timu ya taifa ya Ufaransa.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here